Posts

Showing posts from January, 2025

Wakulima wa kilimo msitu waomba kupatiwa Pembejeo.

Image
   Na Fatma Hamad –Pemba WAKULIMA  WANAOLIMA  KILIMO MSITU katika Shehia za Mjini kiuyu,   Kambini kichokochwe, Mchanga mdogo na Chwale wilaya ya Wete Pemba,  waomba kupatiwa  vitendea  kazi ikiwemo Miche    ili  waweze  kuendeleza  kilimo chao hicho. Wakizungmza na mwandishi wa habari hizi huko vijijini kwao  mwananchi Maryam Khamis Bakar  na Anu Omar Juma , walisema tayari wamesha tayarisha mashamba yao, ila wameshindwa kupanda kutokana na kukosa miche kwa ajili ya kuotesha. ‘’Tayari tumesha tayarisha mashamba yetu vya kutosha, ila tumeshindwa na Miche,’’walisema. Hivyo waliwataka wizara ya Kilimo maliasili, Mifugo  na Uvuvi pamoja Jumuia ya upandaji wa Misitu Pemba CFP kuhakikisha wanawapatia miche ya aina mbalimbali ili waweze kuotesha katika mashamba yao hayo. Kwa upande wao wakulima  Aisha Khamis  na Suleiman Abdala Hamad  wanasema kilimo msitu kitawafanya wanawake kupiga hatua...

Mchango wa wanaume juu ya michezo kwa mtoto wa kike

Image
  NA FATMA HAMAD, Pemba Watoto wa kike nao wana haki ya kupata fursa mbali mbali zitokanazo  na sekta ya michezo, kama wanavyopata watoto wa kiume. Katika ulimwengu wa sasa michezo imekua na fursa nyingi, kama vile ajira, kupata kutembea nchi tofauti tofauti na pia kupata afya bora. Hata Katiba ya Zanzibar ya 1984 katika kifungu cha 6 (2) kinaeleza kuwa, kila mzanzibari kwa misingi ya Katiba hii, ataweza kufaidi haki na fursa zote anazostahiki mzanzibari. Hivyo, ipo haja kwa wanaume kuamka na kutoa fursa kwa watoto wa kike washiriki michezo, ili waweze kujichukulia fursa zitokanazo na michezo. Na hii ilionekana tangu miaka ya zamani ambapo mtoto wa kike alikua akiachwa nyuma katika suala zima la michezo. Katika makala yetu hii, tutaangalia mchango wa wazazi wa kiume katika kuwahamasisha  watoto wa kike kushiriki michezo. JAMII Ali Khamis Kombo mwenye miaka 60 mkaazi wa Sizini Wilya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazi Pemba, anasema tangu alipotia fahamu hakuwahi kuona hata siku ...

WANAHABARI, WADAU ZANZIBAR SASA WATAMANI SHERIA MPYA YA HABARI

Image
                             NA FATMA HAMAD,PEMBA N I miaka 37 tangu S heria ya H abari kufanyiwa marekebisho ,  ingawa bado vipo baadhi ya vifungu katika sheria hiyo vina mapungufu, ambapo  vinaminya uhuru wa habari. Inavyotakikana kila  baada ya miaka 10 sheria huwa nd i o zinahitaji kurekebishwa,  ili kuondosha mapungufu ya vifungu ambavyo vitakua vinaenda kinyume na utekelezaji wa sheria hiyo. Ambapo wakati mwengine ,  sio lazima kusubiriwa miaka 10 bali itakapoonekana tu s heria inamapungufu, basi ni vyema ikarekebishwa. Kwani kufanya hivyo ,  kutasaidia kuweka sawa vifungu vyenye mapungufu na  kuendana na muda na mazingira ya sasa. Ila tukiangalia sheria ya Usajili wa Uwakala wa H abari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanywa marekebisho mwaka 1997, imeshakua kongwe, haiendani na ulimwengu wa sasa. Katika makala hii tutaangalia kifungu cha 30, ambacho kinampa...

TAMWA yatoa agizo kwa wandishi wa habari wa pemba

Image
                        Na Fatma Hamad –Pemba Wandishi wa habari wametakiwa kujikita zaidi vijijini kuibua kero zinazowakwaza wananchi juu  ya masuala ya Afya ya uzazi, ili kuona zinajulikana na kupatiwa ufumbuzi. Wito huo umetolewa na Afisa ufuatiliaji na Tathmini kutoka Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar Mohamed Khatib Mohamed wakati akizungumza na wandishi wa habari na wafanyakazi wa wizara ya afya huko ukumbi wa Tamwa Chakechake Pemba. Amesema bado wananchi hususani wanaoishi vijijini wamekua wakikumbana na vikwazo kadhaa kama vile  kukosekana kwa vituo rafiki kwa mama wajawzito pamoja na upatikananji wa huduma bora za afya. Amesema wandishi wa habari ndio mkombozi wa wasio na sauti, hivyo endapo watafanya  kazi zao ipasavyo na wakaweza kuziibua kero hizo ambazo ni kilio kwa wanajamii, kutasaidia  kupatikana  kwa huduma rafiki na kuepukana na athari zitokanazo na m...

Ukata wa fedha unavyochangia wanawake kuyaogopa majimbo.

Image
Na Fatma Hamad – Pemba Nimewahi  kugombea  mara moja tu,  ila kila nikifiria  kurudi tena jimboni narudinyuma,  kwani sina uwezo kifedha Simulizi ya Fatma Shaaban Mohamed (51) mkaazi wa Kiuyu minungwini Wilaya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,  inatuonesha  ukata wa fedha unavyomkatisha tamaa kuingia tena jimboni katika Uchaguzi wa 2025 Anasema amegombea Udiwani  mwaka 2010 Jimbo la Wingwi Shehia ya Njuguni  Wilaya  ya  Micheweni  Kaskazini Pemba, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. Mama huyo ambae  amezaliwa katika kijiji cha Machengwe Ziwani,  wilaya  ya  Chakechake  Mkoa wa Kusini Pemba. Anasema  amesomea  taaluma  ya  uwalimu  ngazi  ya  Cheti, katika  Chuo  cha  Ualimu  cha   Wiyat  kilichopo  Wete  Mkoa wa Kaskazini  Pemba,  na  ana familia ya watoto saba. Anasema ameanza  harakati za siasa mwaka 2012...

Zanzibar Hiro yawakaribisha kisiwa cha Pemba, Kilimanjaro Star

Image
NA SALIM HAMAD- PEMBA Kocha wa  Timu ya Taifa ya Zanzibar,(Zanzibar Hiro)  Ali Bakari Mgazija mara baada ya kuichapa   bao 1- 0  timu ya Kilimanjaro Star,  katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Michezo Gombani, alisema ushindi huo unatokana na maandalizi mazuri walioyoyafanya. Alisema haukuwa rahisi kuwafunga wapinzani wao kutokana na ushindani uliokuwepo  lakini anashukuru  kwa Vijana wake kufuata maelekezo,  jambo  ambalo  liliweza  kuchangia  kupata ushindi  huo. Alisema bado ni mwanzo wataendelea kujituma zaidi kuona kila mchezo wanashida,  ili kuhakikisha ubingwa wa Kombe la Mapinduzi katika msimu huu wa mwaka 2025 wanalibeba. Alisema anafahamu anakabiliwa na kibarua kizito katika mchezo dhidi ya Burkina Faso utaopigwa Jaruary 6 anaamini,  kwa kasi walioyanayo Vijana wake wataweza kuondoka na alama tatu. ‘’Tunashukuru kwa kumaliza salama niwapongeze wachezaji wangu wamecheza Vizuri kwa kufuata maelekezo tul...

Kilimo msitu tarajio la kuwakomboa wanawake kiuchumi

Image
                            Na Fatma Hamad –Pemba MATARAJIO yangu katika ukulima huu wa  kilimo msitu ni  kujiinua kiuchumi,’’ anasema mnufaika wa mradi wa mabadiliko tabia nchi Asya Abeid Said wa shehia ya Mjini kiuyu wilaya ya Wete Kaskazini Pemba. Anasema lengo hasa la  kujikita katika kilimo msitu ni kulima mazao ambayo yatamsaidia kujipatia  kipato na kuondokana na umasikini, sambamba na kujikinga na athari zitokanazo na mabadiliko tabianchi. Kumbe unapolima kilimo msitu unaweza kuvuna mazao ya chakula,  biashara, sambamba na kuifanya ardhi kuwa na rutba wakati wote. ‘’Nitalima  mazao nitauza, na mingine yatanisaidia kapata chakula cha nyumbani na familia,’’anasema. Hapa matarajio yake ni kulima mazao mengi ya biashara, ili aweze kupata fedha kwa ajili ya kusomeshea watoto wake na kujikimu yale mahitaji ya lazima. ‘’Binafsi nilikwenda kwenye mafunzo Tanazania bara, nikamshuhudia mwan...