Kilimo msitu tarajio la kuwakomboa wanawake kiuchumi
Na Fatma Hamad –Pemba
MATARAJIO yangu katika ukulima huu
wa kilimo msitu ni kujiinua kiuchumi,’’ anasema mnufaika wa
mradi wa mabadiliko tabia nchi Asya
Abeid Said wa shehia ya Mjini kiuyu wilaya ya Wete Kaskazini Pemba.
Anasema
lengo hasa la kujikita katika kilimo
msitu ni kulima mazao ambayo yatamsaidia kujipatia kipato na kuondokana na umasikini, sambamba na kujikinga na athari zitokanazo na mabadiliko tabianchi.
Kumbe
unapolima kilimo msitu unaweza kuvuna mazao ya chakula, biashara, sambamba na kuifanya ardhi kuwa na
rutba wakati wote.
‘’Nitalima mazao nitauza, na mingine yatanisaidia kapata
chakula cha nyumbani na familia,’’anasema.
Hapa
matarajio yake ni kulima mazao mengi ya biashara, ili aweze kupata fedha kwa
ajili ya kusomeshea watoto wake na kujikimu yale mahitaji ya lazima.
‘’Binafsi
nilikwenda kwenye mafunzo Tanazania bara, nikamshuhudia mwanamke kama mimi,
amenunua gari kwa kupitia shughuli zake za kilimo msitu, hivyo na mimi nia
yangu nataka niwasomeshe watoto wangu,’’anasimulia.
Hidaya Khatib Hamad mkulima wa kilimo msitu kutoka Mchangamdogo, anasema kilimo msitu kinaweza kumkomboa mwanamke kiuchumi, kwani anaweza kuvuna mazao tofauti, pia kujiepusha na athari za mazingira.
‘’Unaweza
ukavuna Mdalasini ukauza, ukavuna Ndizi ukapata chakula, na pia kupata elimu ya
utunzaji wa mazingira,’’ anasema Hidaya.
Anajikita
kwenye kilimo mseto ili aweze kujitegemea mwenyewe kimaisha, na kuepuka kukata miti kiholela hapo baadae
kama akihitaji kuni za kupikia.
‘’Unapokua na miti yako shambani utapata kuni,
utaepukana na usumbufu wa kwenda masafa
ya mbali na kuepusha uchafuzi wa
mazingira,’’ anasema.
Kombo Khatib Bakar mkulima kilimo msitu shehia ya Mjini kiuyu Wilaya ya Wete, anakiri kwamba kilimo hicho kitawainua wanawake kiuchumi.
Wanapolima
kilimo hicho mchanganyiko watapata mazao kwa ajili ya kuuza na pia watapata
chakula kwa kipindi karibu miezi 12 ya mwaka.
‘’Watakapolima
mazao kama Mananasi, Maparachichi wanaweza kuuza na kjipatia pesa, na wakilima
mchicha unaweza kuwasaidia majumbani kwao,’’anafafanua.
Aisha Khamis
mwananchi kutoka Mchangamdogo anasema kilimo msitu kitawafanya wanawake kupiga
hatua kiuchumi, kwani wanalima mazao tofauti yakiwemo ya biashara na chakula.
‘’
Tunapolima kilimo hichi tutapata mazao kwa ajili ya chakula, tutapata pesa na
pia tutaifanya ardhi kuwa na rutba nzuri na kuweza kunawiri vizuri mazao,’’anaeleza.
Fatma Saleh
Faki mkulima wa kilimo msitu kutoka shehia ya Mjini kiuyu anasema lengo lake
hasa la kujikita kwenye kilimo hicho, ni kulima mazao kwa ajili ya
biashara.
‘’Mimi
nataka nipande zaidi Mikungu, Mivinje, Minazi, ili nije nipate pesa nimalizie
jingo langu,’’anasema.
Anasema
unapolima miti kama hiyo ya misitu huifanya Ardhi kuwa na rutba, lakini pia
hupelekea mvua kunyesha kwa wingi.
VIONGOZI WA SERIKALI
Afisa mdhamini wizara ya kilimo Umwagiliaji
Maliasili na Mifugo Injinia Idris
Hassan Abdulla anasema kilimo msitu kitawapa faida wanawake, kwani
kitaifanya ardhi kuwa na rutba na kupatikana mazao kwa wingi.
‘’Unapolima
kilimo mchanganyiko kutasaidia kupatikana kwa mvua, na kusaidia kupatikana kwa
mazao kwa wingi,’’anaeleza.
Anasema kama wizara
wamekua wakitoa elimu kwa vikundi mbalimbali ya utunzaji mazingira, ili kuona
wanawake wanapiga hatua kupitia kilimo msitu.
‘’ Ukilima
tembere utapata mboga, ukipanda miembe utavuna embe utauza utapata pesa za
kununua mahitaji mengine ya nyumbani,’’anafahamisha.
WANAHARAKATI
Juma Bakar
Alawi mdau wa masuala ya mazingir, ambae pia aliwahi kushika nafasi mbalimbali
za uongozi katika idara ya mazingira, anasema
wanawake ndio wathirika wakubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi.
Anasema
kupitia mradi huo wa uhifadhi mazingira utawasaidia wanawake kujikwamua na
umasikini.
‘’Kwakweli
jambo wanalolifanya Jumuia ya upandaji
misitu Pemba CFP, na upandi
mistu kimataifa CFI la
kuleta mradi huu wa mabadiliko ya
tabianchi ni jambo jema, kwani wanawake watajipatia mahitaji ikiwemo kuni, na
pesa za kujikimu kimaisha,’’anasema.
Rehema Abrahman Alawi ni
Afisa misitu kutoka Jumuia ya upandaji misitu Pemba
CFP anasema mradi wao
umelenga zaidi kwa wanawake
kwani wao ndio
waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi.
Anasema wamekuwa wakiwapatia elimu pamoja
na miche ya miti mbalimbali wanawake, waweze kulima kilimo msitu kwa
ajili ya kujiinua kiuchumi, pamoja na kuepusha kutokea kwa mmon’gonyoko wa
ardhi.
‘’Unapomwambia
mama apande miti ya misitu katika shamba
lake, atajipatia mahitaji muhimu kama vile kuni, miti ya kujengea, na
kufahamu athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
Omar Hamad
Mjaka katibu wa Jumuia ya ufugaji wa Kuku kisiwani Pemba, anasema kilimo msitu kitawasaidia wanawake
kujikomboa na umasikini.
Wanapolima
mazao mchanganyiko katika mashamba yao, watapata chakula, pesa,
pamoja na kupata hewa safi.
‘’Kwakweli
kilimo msitu kitawafanya wanawake wapige hatua, kwani watavuna mazao kwa ajili
ya chakula, biashara, pamoja na kufahamu
umuhimu wa kutunza mazingira,’’anafafanua.
ATHARI.
Kisiwa cha Pemba ni moja ya visiwa ambavyo vimekua ni muhanga mkubwa wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi, na kwa mujibu wa Afisa Elimu kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Pemba Nassor Ali Salim, anasema endapo kama, hakutochukuliwa hatua za makusudi za kukabiliana na athari zinazotokana na Mabadiliko ya Tabianchi, baada ya miaka 100 kisiwa cha Pemba kitabakia historia, kutokana na maji ya bahari kuingia Nchi kavu.
Anasema kufuatia tatizo hilo la Majichumvi kuingia katika Nchikavu, kunauwezekano mkubwa wa kupoteza Kilomita za mraba 286, sawa na asilimia 28 ya eneo lote la Pemba.
Anasema watu wanaongezeka na Ardhi inaendelea kupungua, hivyo kama hakutochukuliwa jitihada za ziada, juu ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kisiwa cha Pemba kitakua kiko hatarini zaidi, na watu wanaweza kuja kukosa maeneo ya kuishi.
Anasema yapo maeneo yasiyopungua 123 yakiwemo makaazi ya watu pamoja na mashamba yanayotumika kwa ajili ya kilimo, yameathirika kutokana na uingiaji wa majichumvi.
‘’Tuna maeneo mengi yameathiwa na mabadiliko ya Tabianchi kama vile Kojani, Mjini kiuyu, Mkoani pamoja na Micheweni na hayawezi kutumika kwa sasa,’’anasema.
Anasema ni jambo la kushukuriwa kwa Jumuia ya uhifadhi wa misitu Pemba ‘CFP’ na wenzao wa kimataifa ‘CFI’ kwa ushirikiano wa karibu na TAMWA Zanzibar kwa kuamua kuleta mradi huu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa wanawake, kwani wao ndo hasaa waaathirika zaidi wa janga hilo.
Mkurugenzi wa
Jumuia ya upandaji misitu Pemba CFP
Mbarouk Mussa Omar anasema kama hakutochukuliwa
jitihada zozote, juu ya mabadiliko
ya tabianchi, itakuja kusababisha baadhi ya
vijiji kuhamwa kutokana na maji ya bahari kupanda kwenye majumba.
‘’Katika
kijiji cha Mjini kiuyu kila ifikapo mwezi 13,14, na 15 maji ya chumvi yanaigia
ndani ya majumba,’’anasema.
NINI KIFANYIKE
Ili kukilinda kisiwa cha Pemba na athari za mabadiliko tabianchi niwakati kila mmoja kuchukua jitihada za utunzaji wa mazingira ikiwemo kulima kilimo msitu ambacho kinajumuisha miti ya muda mrefu na ya muda mfupi sambamba na miti kuacha tabia ya kukata miti kiholela.
Nairat Abdulla Ali Afisa
kutoka Chama cha
wandishi wa habari wanawake
TAMWA Zanzibar anashauri.
Hili ni jambo jema, kwa jamii
na wanaouendesha mradi huo ambao ni Jumuia ya uhifadhi wa misitu Pemba ‘CFP’
wakishirikiana na wenzao wa kimataifa ‘CFI’ kwa ushirikiano wa karibu na TAMWA
Zanzibar.
Mradi
ambao umefadhiliwa na Serikali
ya Canada na kuridhiwa na serikali ya Mapinduzi, kuona wanawake wamepiga hatua katika suala la kukabiliana na mabadiliko tabianchi.
Kwani lengo hasa la mradi ni
kuwainua wanawake kiuchumi, kupitia mradi huo
wa uhifadhi
wa mazingira.
Uchanganuzi wa Hali Mwaka wa 2023
Uchanganuzi wa Hali Mwaka 2023 inaonyesha kuwa idadi ya watu wanaoenda Mahakamani kukabiliana na janga
la mabadiliko ya taianchi inaongezeka.
Kufikia Desemba mwaka 2022, kumekuwa
na kesi 2,180 zinazohusiana na mazingira,
zilizowasilishwa kwa taasisi za sheria 65 kote
duniani:
Ripoti ya Benki
ya Dunia inasisitiza
umuhimu wa kuunganisha masuala ya tabianchi
katika mipango ya maendeleo
ya Tanzania kupitia Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2050
Ambapo moja ya mkakati wa
ripoti hiyo ni kusaidia jamii
zilizohatarini, kuwa na uwezo
wa kuhimili mishituko ya tabianchi.
Pia ripoti hiyo
imeeleza kuwa kushindwa kuchukuliwa hatua za mabadiliko ya tabianchi,
kunaweza
kupunguza ukuaji wa uchumi wa Tanzania, kwa asilimia nne ifikapo
mwaka 2050.
Aidha kunaweza kusababisha watu Miliono 2.6 kuingia kwenye umasikini, na wengine Milioni 13 kulazimika kuhama makazi yao Nchini.




Comments
Post a Comment