WAANDISHI WA HABARI MSHICHOKE KUDAI MABADILIKO YA SHERIA.

 

Na Fatma Hamad- Pemba

Waandishi wa habari wamehimizwa kuendelea kuzipigia kelele Sheria za habari ziweze kurekebishwa, jambo litalopelekea kuondosha khofu na woga kwa wanahabari hao.

Akizungumza katika mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo juu ya kufanya ushawishi na utetezi kwa Sheria za habari, kwa wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, Afisa programu kutoka Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar Zaina Abdala Mzee, amesema ipo haja kwa wandishi wa habari kupaza sauti zao kwa kuzisemea Sheria hizo, ili kuona kilio chao kimepatiwa ufumbuzi.

Afisa huyo ameyasema hao huko ukumbi wa Tamwa Chake chake Pemba, ambapo amesema endapo kilio cha wandishi wa habari kitazingatiwa na kupatikana kwa Sheria mpya za habari,  kutasaidia wandishi wa habari kufanya majukumu yao bila ya khofu wala woga wowote.

‘’Kama kutapatikana Sheria mpya ambayo itakua haina vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari, kutawasaidia wandishi kufanya kazi zao wakiwahuru,’’ameeleza.


Akitaja vifungu ambavyo vimekua ni kandamizi kwa wandishi wa habari, Mkufunzi wa Mafunzo hao Haura Shamte  kutoka Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania [TAMWA]  Zanzibar amesema ni kifungu cha 4, na kifungu cha 27[1] vya sheria ya Usajili wa wakala wa habari Magazeti na vitabu No 5 ya mwaka 1988 iliyo rekebishwa na sheria no. 8 ya mwaka 1997.

Ameendelea kusema kuwa vifungu vengine ambavyo vimekua ni kikwazo kwa wandishi wa habari pamoja na vyombo vya habari ni kifungu cha 27 (1) na 27 (2) vya sheria ya Tume ya Utangazaji No. 7 ya mwaka 1997 kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria No 1 ya mwaka 2010.

Aidha ameendelea kusema kuwa  wakati umefika kwa wanahabari  kufanya utetezi kwa kina juu ya Sheria hizo, ziweze kufanyiwa marekebisho na kuona zinaendana na wakati.

‘’Kwa kweli sheria yetu imeshapitwa na muda tunaomba ifanyiwe marekebisho ili kuondoa vifungu ambavyo vinakinzana na uhuru wa vyombo vya habari, amesema.



Nao waandishi waliopata mafunzo hayo wameahidi kuendeleza mapambano ya kufanya ushawishi, ili kuona mamlaka zinazohusika na masuala ya Sheria, zinatimiza azma ya wandishi wa habari ya kupata Sheria mpya ambayo itakua rafiki kwao.

                           

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO