Jumuiya za vyama vya siasa, muarubaini wa kuwasaidia wanawake kwenye uongozi
MWENYEKITI
wa CUF Mhamed Haji Kombo, wa Chake chake
akiri kuwa uanzishwaji wa jumuia za wanawake ndani ya vyama vya siasa,
zimesaidia kwani zimewaamsha wanaume kufahamu kwamba, haki ya kugombea ni kwa
wanachama wote.
Aanasema jumuia za
wanawake zimezaa matunda kwani wanawake katika Chama chao wamekua na uthubutu
wa kugombea nafasi za ungozi, ambapo ngazi za kitaifa viongozi wengi ni wanawake.
’ ‘Wamekuwa wakipata
elimu na mafunzo mbali mbali kwenye
jumuia zao, na ndo maana wakawa na uthubutu huo wa kuhodhi nafasi za uongozi,’’
Amesema Mohamed wakati wa mahojiano.
Mwenyekiti wa
Chama cha ACT WAZALENDO Mkoa wa Kusini Pemba kichama, Saleh Nassor Juma anasema
mchango wa Ngome za Wanawake ni mkubwa kwani zimewafanya wanawake waondokanae
na hofu ya kugombea na kushika nyadhifa za uongozi.
‘’Kwa kweli hizi Jumuia za wanawake kwenye
vyaama zimewatoa hofu wanawake, maana ukiangalia kwenye kamati yetu ya uongozi ya Mkoa Chake chake takribani asilimia 50 ni wanawake, nahii ni
kutokana na elimu wanayopatiwa,’’ ameeleza.
Katibu wa Chama
cha Mapinduzi CCM Wiala ya Micheweni
Khamis Juma Omar anasema lengo kuu la kuanzishwa kwa jumuiya za wanawake ni
kuonesha umuhimu wa mwanawake na kuona kwamba
hawajaachwa nyuma katika harakati za kisiasa.
Amefahamisha kuwa
wengi wa wanawake wamekuwa na ujasiri wa kujingiza majimboni na kugombea hii ni kutokana na kuwanzishwa kwa jumuiya
zao hizo za wanawake .
Khamis amesema
jumuiya ya wanawake (UWT) ya chama chao wamekuwa wakipatiwa mikopo serikalini.
‘’Tumekua
tukiwasimamia na kuhakikisha wanapata mikopo na mfuko wa uwezeshwaji wanawake
kiuchumi ili kuona wanaendesha shughuli zao ambazo zitakazowsaidia katika
harakati zao za uongozi,’’
Uwepo
wa jumuia za wanawake ndani ya vyama vya siasa, ndio tenuri la wanawake,
kujengewa uthubutu wa kugombea nafasi zilizoonekana ni za wanaume pekee.
WANACHAMA WA VYAMA VYA SIASA
Shaame Suleiman
Shaame ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM mkaazi wa Sizini Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,
anasema anakumbuka katika wilaya yao ya Micheweni nafasi ya uwenyekiti kwenye
Chama hicho ilishawahi kushikwa na mwanamke.
‘’Wanawake
wanapatiwa uwezeshwaji wa mafunzo ili waweze kujiamini, pamoja na mikopo ya
ujasiariamali kupitia kwenye Jumuia zao hizo za Umoja wa
Akinamama,’’amemalizia.
Jumuiya za
wanawake ndani ya vyama vya siasa hazipo tu kwa ajili ya kuvinufaisha vyama
bali vimekua ni mkombozi mkubwa kwa wanawake.
Hili
limethibitishwa na Tumu Mwali Masoud (40) ambae amelelewa na jumuia ya wanawake
(UWT) ambapo kwasasa amekua na uthubutu wa kuingia jimboni na kugombea.
Tumu anasema
jumuiya imemnufaisha kwani alishapata mafunzo mbalimbali yakiwemo ya Uongozi.
Anasema Katika
uchaguzi uliopita wa 2020 aliingia kwenye uchaguzi na kugombea jimbo kwa upande
wa uwakilishi,kwa vile alijiona anaweza kwani alikua tayari alishandaliwa na
Chama chake.
’’Nililelewa na jumuia ya wanawake wa chama changu cha Mapinduzi CCM, na ilinijengea uthubutu na
mwaka 2020, niliingia jimboni na kugombea,’’
anasimulia Tumu.
Ziada Khalfan Saleh, (48) mwanachama wa Chama cha Tanzania Labour Party –TLP, anasema anapata semina za ndani na nje ya kisiwa cha Pemba, jambo linalomfanya kujuana na watu tofauti tofauti na kubadilishana mawazo juu ya uongozi kwa mwanamke.
‘’Tunapelekwa kwenye mafunzo ili tuweze kujiamini na kua
Viongozi bora,’’amesema
ASHA Mohamed Ali, (45 ) mkaazi wa Wawi Chake Chake ambae ni mwanachama wa
Chama cha United DemockratiC Party –UDP, aliejiunga na jumuia ya wanawake tokea mwaka 2012.
Amesema mchango wa jumuiya za
wanawake ni mkubwa, na ndio sehemu ambayo kupitia jumuiya hizo, amepata nafasi
ya kuteuliwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa
UDP Mkoa wa Kusini Pemba.
‘’Jumuiya
imenisaidia kwani baada ya kuonekana nafanya vizuri kwenye majukumu ya jumuiya,
nimeteuliwa kupewa uongozi wa kwenye chama,’’Amesema Asha ambaye ameona fursa
kuwa kwenye jumuiya hizo.
VIONGOZI WA JUMUIYA ZA WANAWAKE
Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanawake Tanzania – UWT Wilaya ya Micheweni, Mkitu Hassan Mwalim anasema
katiba ya jumuiya yao, imetekelezeka kwa Chama cha Mapinduzi kimekua
kikiwapatia ruzuku,pamoja na mafunzo ya uongozi.
‘’Binafsi nimeandaliwa
kuptia jumuia nasasa nimekua kiongozi, na nawaelimisha wananchi wangu wanake
ili nawao wawe na uthubutu wa kusimama popote na kzungumza, pamoja na
kugombea,’’amesema.
Batuli Mussa
Sharif, (46) Naibu katibu wa idara ya Uchaguzi (Oganazitio) Zanzibar kutoka
Chama cha ACT WZALENDO mkaazi wa Kijichame Wilaya ya Micheweni Pemba, amasema jumuiya
kwenye chama chao jumuiya inaitwa Ng’ome ya wanawake ,amesema jumuiya hizo za
wanawake zimekuwa zikiwasaidia kwani
wanapata mafunzo kuhusu kujiamini na kuondokana na woga.
‘’Binafsi baada ya
kupata mafunzo nimeelimika na nina
uthubutu wa kusimama popote na nikazungumza, na najitayarisha mwakani kuingia
kwenye jimbo kugombea,’’Amemalizia Batuli.
MWANAHARAKATI
Mwanaharakati wa
masuala ya kupambana na haki za wanawake na watoto Wilaya ya ChakeChake
Kisiwani Pemba Amina Omar Mselem,anasema ni
jambo jema uwepo wa jumuiya za wanawake kwenye vyama kwani wengi ambao
wamekua na uthubutu wa kusimama mbele za watu na kujieleza ni wale ambao
wamepitia kwenye jumuiya hizo.
‘’Kiukweli jumuiya
zina mchango mkubwa kwani wengi wa wanawake ambao wanajingiza kwenye
kinyanganyiro cha kuwania majimbo ni wale ambao wanatoka kwenye Ngome kwani
elimu inakuwa inatolewa vya kutosha ili waweze kujiamini’’.Amemalizia Amina.
TAKWIMU
Takwimu za uongozi za
vyama vya siasa zilizokusanywa mwaka 2024 na afisi ya msajili wa vyama vya siasa
Tanzania, zimeonesha hadisasa kunavyama vitatu tu ambavyo wenyeviti wanawake ambavyoni
CCM, ACT_ wazalendo na SAU.
Aidha kwa nafasi za Makatibu
Wakuu pia nivyama vitatu (3 ) tu ndio vyenye Makatibu Wakuu wanawake ambavyo ni
CCK, UNDP na NCCR_Mageuzi.
Kwa Pemba ambako kuna Wilaya nne na Mikoa miwili,
ni vyama
vinne (4) tu, ndivyo
vinamakatibu wanawake wa
mikoa, ambavyo ni, TLP, NRA,
NLD na CHAUMA .
Kwa mujibu wa
ripoti Maalumu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, iliyotolewa na Chama Cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanazania
Zanzibar (TAMWA) imesema kuwa, nafasi ya uwakilishi kwenye majimbo 50 ya
Zanzibar wanawake ni asilimia 16 ambao ni nane tu.
Kwa upande wa Ubunge
wanaowakilisha Zanzibar wanawake ni, wanne sawa na asilimia 8, Mawaziri wakiwa
ni sita sawa na asilimia 33 na Makatibu wakuu ni saba sawa na asilimia 39.
Kwa upande wa Wakuu
wa Mikoa mwanamke ni mmoja tu sawa na asilimia 20, Wakuu wa Wilaya ni wanne
sawa na asilimia 36 na
Masheha wanawake 81 sawa na asilimi 20, kwenye shehia 388 ya masheha wote Zanzibar.
SERA YA CHAMA CHA MAPINDUZI
Sera ya Chama cha
Mapinduzi ni kuongoza umma wa watanzinia katika ujenzi wa uchumi wa kisiasa
utakaoleta maisha bora ya wananchi kwa kuwawezesha kiuchumi.
KATIBA YA (UWT) TANZANIA
Katiba ya jumuia
ya umoja wa wanawake Tanzania –UWT ya mwaka 1978 toleo la mwaka 2017, imesema
UWT itapata ruzuku kutoka Chama cha Mapinduzi.
Comments
Post a Comment