Adaiwa kubaka mtoto wa miaka mitatu

 


Na Fatma Hamad -  Pemba

MAHKAMA ya Mkoa iliyopo Wete Pemba imempeleka rumande Rashid Ali Hamad (31) mkaazi wa Kiuyu kipangani, anaedaiwa kumbaka mtoto wa miaka mitatu.

Baada ya mtuhumiwa huyo kupanda katika kizimba cha Mahkama hiyo, alisomewa shauri lake, na Mwendesha Mashtaka wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Heri Hassan Omar, ambapo alikataa kata kata.

Pp Heri aliambia Mahkama kuwa kwa vile mshitakiwa amekataa shitaka lake, nivyema kesi ikaghairishwa na ipangiwe sikunyengine kwa ajili ya kusikiliza mashahidi, kwani tayari upelelezi ulishakamilisha.

‘’Mheshimiwa Hakimu tunakuomba tuipange siku nyengine, kwa vile ushahidi umeshakamilisha, ili tuite mashahidi,’’alidai.

Nae Hakimu  Zuwena Mohamed Abdulkadir alikubaliana na Mwendesha Mashtaka, ambapo kesi itarudi Mahkamani hapo Novemba 18 mwakahuu, huku akimtaka mtuhumiwa abakie rumande hadi tarehe hiyo.

Imedaiwa Mahkamani hapo mtuhumiwa huyo Sebtemba 11 mwaka huu katika kijiji cha Kiuyu kipangani alimbaka mtoto wa miaka mitatu, jambo abalo ni kosa kinyume na kifungu cha  108  (1), (2),(e) na 109 (1) vya sheria ya adhabu namba 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.


Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI