Dawa za kulevya zamsababishia kwenda Jelamiaka 7
NA FATMA HAMAD,PEMBA Ridhwan Mkongwe Sharif mwenyeumri wa miaka 38 mkaazi wa Kipange Konde Pemba,ameanza maisha mapya katika chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka saba, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na misokoto 50 ya dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 210.5. Mapema Hakimu wa Mahkama ya Mkoa Wete Zuwena Mohamed Abdulkadir alisema, baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kuona kwamba hauna chembe ya shaka, mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo. ‘’Kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wetu tumejirisha na kuona ushahidi uliotolewa ni wa ukweli hivyo mahkama imekukuta na hatia mshitakiwa,’’ alisema. Mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka D...