MSHITAKIWA WA SHITAKA LA ULAWITI APATA DHAMANA


 

 

NA FATMA HAMAD,PEMBA

MAHKAMA ya MkoawaKaskazini Pemba imempadhamana mtuhumiwa Faki Hamad Faki 35 mkaazi wa Kambini Mchangamdogo anayakabiliwa na mashitaka ya kutorosha na kumlawiti  mtoto wa kiume  mwenye umri wamiaka 12.

Hakimu wa mahakama hiyo Zuwena Mohammed Abdalla alisema mahakama imeamua kumpa dhamana mtuhumiwa ni kutofika kwa mashahidi mahkamani kwa ajili ya kutoa ushihidi dhidi ya shaurihilo.

Alifafanua kuwa kwa, mujibu wa kifungu cha 152 cha sheria namba 7 yamwaka 2018, sheria ya jinai inaeleza kwamba kama hakuna shahidi yoyote aliyefika mahakamani na kutoaushahidi kwa muda wa miezisita , mtuhumiwa apewe dhamana.

“Kutoka na na kifungu hicho, Mahkama inampa dhamana mtuhumiwa   kwa masharti ya    shilingi laki tano taslimu  na wadhamini  wawiliwakiwa na kopi zakitambulisho cha Mtanzania au Mzanzibar, naakishiwa mtuhumiwa atarejea rumande” alieleza.

Mapema mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Mohammed Ali alisema shaurilipo kwaajili ya kusikiliza mashahidi ila hatujapokea shahidi.

“Mheshimiwa hatuna shahidi aliyefika leo na wala hapana tataarifa za kuhusu mashahidi kutofika kwa hiyo naomba kesi hii ipangiwe siku nyengine na barua za witozitolewetena”alisema.

Kwa upande wake mtuhumiwa huyo aliomba mahkama kuiondosha kesi  hiyokwani mashahidi hawafiki mahakamani kutoa ushahidi wao na  kesi imekuwa ni yamuda mrefu.

“Ni siku nyingi sana nimekaandani ,hivyo naomba kesi ifutwe kwani mashahidi wameshindwa kuja kutoa ushahidi”alishauri.

Mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo septemba 30, mwaka 2023 saakumi na mbili na dakika kumi  zajioni  ambapo alimtorosha mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka12.

Sikuhiyohiyo mjira ya saa 12 na robo za jioni alimlawili mtoto huyo wakiume jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu cha 115 (1) cha sheria ya adhabu namba 6 yamwaka 2018 sheriaza Zanzibar

Mwisho.

 

 

 

 

Comments