RUSHWA MUHALI BADO YAENDELEA KUOTA MZIZI KATIKA JAMII

 

 
 
NA FATMA HAMAD,PEMBA

Mwakilishi wa Viti malumu Mkoa wa Kaskazini Pemba Hindi Hamad Khamis amewataka Wananchi wa Micheweni kuwacha tabia ya kuyafumbia macho matukio ya udhalilishaji jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa matendo hayo katika Jamii.

Mwakilishi huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Chamboni Micheweni Pemba katika mkutano maalumu ulioandaliwa na Jumuia ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Micheweni wa kutoa elimu kwa Jamii juu ya masuala ya udhalilishaji kwa wanawake na Watoto.

Alisema bado wapo baadhi ya watu wanaendelea na tabia ya rushwa  muhali  juu ya matendo ya udhalilishaji, kwa kukhofia ugomvi katika familia zao, jambo linalowafanya  watoto kuishi kwa wasi wasi.

‘’Niwaombe wananchi wenzangu wa micheweni tuache muhali tusiogope unapodhalilishiwa mwanao toa mashirikiano katika vyombo vya sheria hata kama ni jamaa yako usifiche,alisisitiza’’

Alifahamisha kuwa Mkoa wa Kaskazini Pemba bado hali ya udhalilishaji iko juu, hivyo ni wakati kwa wanajamii  kukaa chini na kushirikiana bega kwa bega na Serikali kuhakikisha wanawadhibiti wahalifu wa matukio hayo ili kukomesha matendo hayo ambayo ni hatari kwa Jamii na hata Taifa kiujumla.

 
 Mapema Msaidizi wa sheria wilaya Micheweni Said Salim Khamis aliwataka wananchi hao kuvunja ukimya kwa watoto wao na kuwafahamisha madhara ya udhalilishaji ili waweze kujilinda na masuala hayo.

‘’Wazazi hali imekua tete tuiwaonee haya watoto wetu tukaeni nao karibu na  tuzungmze nao,ili waweze kufahamu maana ya udhalilishaji na waweze kujilinda,alifahamisha’’

 
 Kwa upande wake Afisa dawati la Jinsia kutoka kituo cha Polisi Micheweni Mohamed Ali Hamad aliwashauri wazazi na walezi kuwapa elimu ya kujitambua watoto wao ili wawe na madili mema anayoyaridia Allah (S,W).

 Nao baadhi ya Wananchi waliohudhuria mkutano huo waliomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoa adhabu kali kwa Mwanamme na Mwanamke watakaokamatwa wamefanya kitendo cha udhalilishaji,na isiwe kwa mwanammetu,  kwani inaweza ikawa muarubaini wa kupunguza matukio hayo.

‘’Twaiomba Serikali kama mwaname  atafungwa mika 15 basi na mwanamke nayeye afungwe japo mika 10, walisema’’.


 


Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’