WAUMINI WANAOTARAJIWA KWENDA KUTEKELEZA IBADA YA HIJA WAPEWA DARSA


                                       NA FATMA HAMAD,PEMBA

Mahujaji  wanaotarajia kwenda kutekeleza ibada ya Hijja  katika mji mtukufu wa Makka hivi karibuni wametakiwa kufuata mafunzo waliopewa  na Taasisi za Usafirishaji  Mahujaji, kwa kutojihusisha na Vitendo visivyokubalika, ikiwemo kusengenya na ushirikina .

Wito huo umetolewa  na Afisa Mdhamin ofisi ya Makamo wa kwanza wa rais Ahmed Abuu Bakar  Mohd  huko Skuli ya Madundu Sekondari Kisiwani Pemba  katika hafla ya kuwaaga Mahujaji  watarajiwa kutoka taasisi ya Tatwawwule tawi la Pemba.

Alisema katika  kufanya ibada ya Hijja kuna hitaji umakini kwa kujizuia na mambo machafu na kufanya mambo ya msingi ambayo yatapelekea kufanikiwa kutekeleza ibadada hiyo.

Alisema kuna mambo mengi yanafanyika Makka mengine yakiwa mazuri na mengine yakiwa mabaya lakini kikubwa ni kufuata maelekezo na masharti kwa kuangalia vitu wanavopaswa kuvifanya.

‘’Niwaombe Mahujaji mufuate mafunzo mliopewa yanayolenga kufanikiwa kwenye ibada yenu ya Hijja kule kuna mambo mengi yanafanyika lakini mnapaswa kujiepusha, navyo vitu hivyo ni kama kusengenya na ushirikina vitu hivyo vinaweza kuharibu ibada zenu jiepusheni’’alisema .

Hata hivyo Ahmed aliwataka Mahujaji hao kuomba Msamaha kwa Majirani Ndugu na Marafiki waliokosana nao ili kwenda kutekeleza ibada hiyo kwa wepesi na kufanikiwa kwenye ibada hiyo.

‘’Haiwezekani unataka kwenda Makka lakini kuna watu ulikosana nao lazima uwatafute uwaombe Msamaha waridhie na kuwapa taarifa ndugu jamaa na marafiki kuelekea kwenye safari hiyo’’alisema.

Katibu wa Jumuiya Tatwawwule Zanzibar, Hasnuu Habibu Ali  alisema Mahujaji hao waliwapatia mafunzo ya wiki moja kwa ajili ya kujua namna ya masharti na misingi ya ibada ya   Hijja  katika Mji wa Makka ili waislamu waweze kukamilisha vizuri Nguzo ya tano ya Uslamu.

  Jumla ya mahujaji 103  kutoka taasisi ya Tatwawwule Zanzibar wanarajia kwenda kutekeleza ibada ya Hijja  kuanzia mei 30 ambapo kati ya hao 34 ni kutoka Kisiwani Pemba.

 







 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO