WANAWAKE WENYE ULEMAVU WAOMBA USHIRIKISHWAJI KWENYE MICHEZO
NA FATMA HAMAD,PEMBA
Katika kuelekea siku ya mtoto wa Afrika duniani Makamo mwenyekiti wa Jumuia ya wanawake wenye ulemavu Zanziba Hidaya Mjaka Ali ameitaka jamii kuwashirikisha watoto wa kike wenye ulemavu katika harakati mbali mbali ikiwemo Michezo ili nawao wapate fursa zilizomo katika Nchi.
Akizungumza na mwandishi wa habari huko ofisini kwake Mkanjuni Chake Chake Pemba anasema watoto wa kike wenye nawao wana haki ya kushiriki michezo kama watoto wengine.
Alisema jamii imekuwa akiwachukulia watoto wenye ulemavu kwamba hawawezi kushiriki michezo kutokana na ulemavu wao.
‘’Ukimuelekeza, na ukimjenga vizuri mtoto mwenye ulemavu mboana anaweza akacheza na akafanya vizuri,’’alisema.
Alisema ni wakati kwa jamii kuondokana na itikadi potofu, na badala yake wawashirikishe watoto wenye ulemavu kwenye michezo ili wajipatie kipato kupitia michezo
Aidha bi hidaya alisema bado miundombinu ya michezo haiko rafiki kwa wanawake wenye ulemavu.
Kwa upande wake Fatma Mkubwa Mussa mwenye ulemavu wa viungo mkaazi wa Mkoani alisema watoto wenye ulemavu nawao wana haki ya kushiriki michezo, hivyo nibudi nawao washirikishwe ipasavyo kama watoto wengine wasio na ulemavu.
Afisa Mdhamini wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau anasema wizara imo kwenye mkakati wa kuboresha miundombinu ya michezo ikiwemo viwanja ili kuona watu wenye ulemavu nawao wanaingia kwenye michezo.

.jpg)
Comments
Post a Comment