WANAOJISHUGHULISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA CHA MOTO KUKIONA
Na Is-haka Moh`d-Pemba
Waziri waNchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Harusi Said Suleiman amewaomba Wazazi/Walezi Visiwani Zanzibar kufuatilia kwa karibu nyenendo za watoto wao ili kuwalinda kutumbukia katika janga la utumiaji wa dawa za kulevya.
Waziri Harusi ametoa ombi hilo wakatia kifungua kongamano la siku ya maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya duniani ambapo kwahapa Zanzibar Kitaifa yameanzimishwa leo Juni 27 katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Alisema utumiaji wa dawa za kulevya umekuwa ukiathiri kwa kiasi kikubwa kwa vijana walio na umri kati ya miaka 9 na 45 ambapo vijana wengi huanza kutumia matumizi ya dawa za kulevya wakiwa katika Skuli za msingi na Sekondari.
Amesema endapo wazazi na walezi watasimamia wajibu wao ipasavyo katika kusimamia malezi ya vijana na watoto kutasaidia kupunguza idadi ya waathirika wa matumizi ya madawa ya kulevya iliyofikia zaidi ya elfu 15 kwa sasa visiwani Zanzibar.
Waziri Harusi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na juhudi mbalimbali za udhibiti utumiaji wa dawa za kulevya ikiwemo kutoaelimu kwa jamii juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya kwataifa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar Kanali Burhan Zuber Nassor ameitaka jamii kuchukua tahadhari kabla ya kupata madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya na kutaka mapambano ya dawa za kulevya yaanzia katika ngazi za familia.
Alisema kuwa Serikali kupitia Mamlaka hiyo itachukua hatuakali kwa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwemo kufilisi mali zao kwa mujibu wa sheria, hivyo amewaomba wananchi kutoa mashirikiano kwa mamlaka hiyo kwa kutoa taarifa za wanaofanya biashara hiyo.
“Matumizi ya dawa za kulevya yanaatharinyingi ikiwemo kudumaza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana, alisema’’
Alisema haipendezi kuona watoto na vijana wadogo walio katika Skuli za msingi, sekondari na vyuo vikuu wakitumbukia kwenye janga la matumizi ya dawa za kulevya, hivyo Mamlaka itaongeza juhudi za mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
Akiwasilisha mada ya Uhalifu wa dawa za kulevya Haji Makame Omar kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya alisema dawa za kulevya bado ni tatizo linaloendelea kuiathiri jamii, hivyo
amewagiza viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu katika maeneo yao ili kuona Vijana wanaiepusha na vitendo hivyo viovu.
‘’Viongozi wa dini nyinyi mnanafasi kubwa katika jamii hivyo toeni elimu katika vikao vyenu, ili jamii ifahamu madhara ya dawa za kulevya,alisema’’
Kwa upande wake Othman Said Juma kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ameitaka jamii kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kutoa tarifa pale watakapoona kuna viashiria vya uzwaji wa dawa za kulevya.
Madhimisho ya siku ya kupiga vita Matumizi na Usafirishaji wa dawa za kulevya hufanyika kila June 26 ambapo ujumbe wa mwaka huu Ushahidi uko wazi wekeza katika kukinga.




Comments
Post a Comment