WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPATA MATIBABU





                                 NA FATMA HAMAD,PEMBA

Wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kambi ya uchunguzi na matibabu iliyopo Micheweni uwanja wa kwa mshaame mata, ili waweze kuchunguzwa na kujulikana matatizo yao na kupatiwa tiba.

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib wakati akizungumza na wananchi wa mkoa  huo katika uzinduzi wa kambi ya Uchunguzi na Matibabu iliyoandaliwa na tasisi ya Zanzibar Maisha bora Fondation huko Micheweni Pemba alisema matibabu hayo yatatolewa bure kwa wanachi wote.

Alisema lengo la Serikali  ya Mapinduzi ni kuona wananchi  wanaishi wakiwa na afya njema, hivyo ni vyema kila mwenye matatizo kufika katika kambi hiyo ili aweze kuchunguzwa na kupatiwa huduma bora za afya.

‘’Taifa bora linajengwa na jamii iliyo bora, hivyo msione tabu kuja kupata tiba kwani ni bure,’’alisema

Alisema endapo kama kutakuwa na wagonjwa watashindikana kupatiwa matibabu, katika kambi hiyo watapewa rufaa na kwenda kutibiwa sehemu nyengine.

Aidha kwa upande mwengine aliwataka wananchi hao kufanya mazoezi kwa wingi ili waimarishe afya zao, na waondokane na maradhi nyemalezi.




Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa tasisi ya Zanzibar Maisha bora Fondation Fatma Fungo alisema katika mikoa ya Kaskazini ya visiwa vya Zanzibar  imegundulika kuwa takriban asilimia 48 ya  wanawake  wenye umri wa kubeba ujauzito wamekuwa  wakikabiliwa na changamoto ya lishe duni, hali ambayo inaleta athari kwa mtoto anaezaliwa.

‘’Kambi hizi tumeziweka zaidi katika mikowa ya kaskazini ili kutatua tatizo hilo la lishe katika mikoa hiyo,’’alisema

Alisema mwenyekiti wa tasisi hiyo Maryam Mwinyi alisema atahakikisha anapambana na changamoto hiyo ya lishe ili kuona hakuna  mtoto anaezaliwa na udumavu.


Afisa mdhamini wizara ya afya Pemba Khamis Bilali Ali alisema katika kipaombele cha wizara ya afya ni kuona wanaboresha huduma za afya ya msingi kwa wananchi wote.

‘’Tumejipanga, Kutoa huduma bure, kuanzia kwenye vipimo na madawa,’’alisema.

Aidha aliwata wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchangiaji wa damu sama, kwa ajili ya kuisaidia jamii.

Katika  kambi hiyo jumla ya watu 50 wanatarajiwa kupatiwa matibabu ya maradhi mbali mbali ikiwemo Saratani ya shingo ya mlango wa kizazi, Saratani ya matiti, huduma za afya ya mama na mtoto, macho, Koo, Pua, upimaji wa vipimo vya kimaabara, huduma rafiki kwa vijana pamoja na chanjo ya Uviko 19. 


   

 

  

 


 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO