UVCCM YAOMBA KUFUNGIWA KWA MTANDAO WA KIJAMII WA X

                                         


                                   NA FATMA HAMAD,PEMBA.

Umoja wa vijana  (UVCCM)  Mkoa wa Kaskazini Unguja umeiyomba  Serekali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar,kuuchukulia  hatua mitandao ya kijami X (TWITTER) ikiwemo kuufungia ambao wamedai unakwenda  kinyume na madili ya vijana wa  Tanzania.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Ismail Ali Ussi alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema Serikali inapaswa kuangalia kwa karibu na  kuufungia mtandao huo  kawani unatoa maudhi ambayo si mazuri kwa Vijana wa Taifa hili  wakihofia kuaharibika kwa Vijana.

Alisema  mtandao huo unaweza kupelekea kuporomoka kwa madili ya vijana wa taifa hili kutokana na video zinazo rushwa na mtandao huo zinazoenda kinyume na madili .

Alisema mtandao huo kama huukuangaliwa unaweza kuleta taharuki  na kusababisha kuwepo migogoro kwa Vijana hivyo wameomba Serikali kuchukua hatua za kuufungia.

‘’Tunaiyomba Srikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar,kuchukua hatua za kuufungia mtandao wa x kwani unakwenda kinyume na maadili ya Vijana wa Tanzania’’alisema.

Hata hivyo aliwataka Vijana kuwa makini katika matumizi ya Mitandao ya  Kijamii kwa kutojihusisha kurusha vitu ambavo havina nafafasi kwenye Jamii. 


 

 


Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO