UNYANYAPAA BADO NI KERO KWA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU
NA FATMA HAMAD,PEMBA
Jamii imetakiwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa wagonjwa wanaouguwa ugonjwa wa kifua kikuu, jambo ambalo linasababisha watu kuwa na khofu ya kujitokeza Hospitalini na kupatiwa matibabu.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa elimu habari na mawasiliano katika kitengo shirikishi cha ukimwi, homa ya ini, kifua kikuu, ukimwi na ukoma kisiwani pemba khalfan khamis khalfan wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Chake chake Pemba.
Alisema licha ya elimu inayoendelea kutolewa katika jamii lakini bado kunachangamoto ya kunyanyapaliwa kwa wagonjwa wanaougua kifua kikuu kutoka kwa familia zao, hali ambayo inapelekea kuenea kwa maradhi hayo.
‘’Jamani ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa kama maradhi mengine hivyo tusiwatenge watu wetu kwa sababu eti wamepata tatizo hilo,alisema.
Aidha kwa upande mwengine amewataka watu watakaogundulika na ugonjwa wa kifua kikuu kutumia dawa za Hospitalini na sio kukimbilia kwa waganga wa Jadi, jambo ambalo linapelekea athari kubwa kwa afya zao.
‘’Nikweli watu wengi wanamini itikadi potofu kwamba kifua kikuu ni maradhi yanayotokana na ushirikina, hilo sio kweli bali ni ugonjwa kama ugonjwa mwengine ambao unatibika,alieleza.
Hivyo alisema nivyema mtu atakapojiona na dalili za ugonjwa huo akimbilie kituo cha Afya kupatiwa tiba mbadala.
Kwa upande wake Mratibu wa jumuia binafsi Zanzibar Mwana Bashir alizitaka jumuia zinazofanya kazi na kitengo hicho shirikishi wasivunjike moyo bali waendelee kutoa Elimu kwa jamii juu ya ugonjwa wa kifua kikuu ili kuona unaondoka Nchini.
Nae Mratibu wa kitengo shirikishi cha ukimwi, homa ya ini, kifua kikuu, ukimwi na ukoma kisiwani pemba Khamis Hamad Ali alizitaka asasi hizo kufanya kazi kwa mashirikiano ya hali ya juu ili waweze kuibua wagonjwa na kupatiwa matibabu sahihi na kwa wakati.
Jumla ya wagonjwa 63 wa kifua kikuu waliibuliwa na kuendelea na matibabu katika kipindi cha mwaka jana 2023 kisiwani Pemba.



Comments
Post a Comment