WASAIDIZI WA SHERIA PAMOJA NA WANDISHI WA HABARI WAOMBWA KUJIKITA VIJIJINI NA KUIBUA KERO ZA WANANHI.






NA KHADIJA OMAR PEMBA                                                                                                                          WAANDISHI wa habari  na  watetezi wa haki   za binadamu wametakiwa kuzitumia  nafasi walizonazo  kuelimisha  jamii  na kutetea masuala ya uvunjifu wa haki za binadamu   ikiwemo vitendo vya udhalilishaji.

Akizungumza katika  hafla ya ufungaji  wa mafunzo ya siku nne, yaliyo washirikisha wandishi wa habari , watetezi wa haki za binadamu na wadau mbali mbali Siti Habibu Mohamed  kutoka                             afisi ya shirika la msaada wa kisheria   Pemba (ZALHO)alisema ni wajibu wa wandishi wa habari kuibua na  kutetea masuala ya uvunjifu wa haki za binadam katika jamii ili ziweze kueleweka na kupatiwa ufumbuzi.

Alisema kuwa, wandishi  wa habari  na watetezi wa haki za binadamu  wana kazi kubwa katika  kuibua na kutetea   masuala ya uvunjifu wa haki za binadamu katika jamii  kutokana na  uelewa mdogo wa wanajamii.

Alieleza kuwa, kuwepo kwa shirika la msada wa kisheria kutawawezesha  wananchi kuzifahamu haki zao na kuwa na uthubutu wa kuzitetea pale watakapoona zimevunjwa.

Nae  Afisa  habari  kutoka  Chama cha wandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) ofisi ya Pemba   Gaspa Charles alisema  kuwa endapo wandishi wa habari watandika na  kuripoti habari  kwa kuzingatia miko na madili ya kazi yao itaepusha kuandika habari zenye migogoro katika jamii.

Nao baadhi ya  washiriki wa mafunzo hayo  walisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kutatua masuala ya uvunjifu wa haki za binadamu katika jamii zao.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mwavuli wa asasi za kiraia Pemba,(PACSO)  yaliwashirikisha wandishi wa habari , wadau na watetezi wa haki za binadamu  yamedhaminiwa na UNDP.

 


Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO