WANDISHI WA HABARI WAKUMBUSHWA KUANDIKA HABARI ZINAZO HUSU HAKI ZA BINADAMU

NA FATMA HAMAD, PEMBA`

WANDISHI wa habari wametakiwa kuwandika na kuripoti habari zinazohusu  masuala ya haki za Binadamu,  ili  jamii  ifahamu  haki  zao, wajibu wao, na kuweza kuzitetea pindi wakiona  zimevunjwa.

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la mtandao wa asasi za kiraia Pemba [Pacso] wakati akifungua mafunzo ya kuwahamasisha wandishi kuandika habari zinazo husu masuala ya haki za binadamu  yaliyofanyika Ranzi Vitongoji Chake chake.

Alisema wandishi wa habari wana nafasi kubwa katika kuielimisha jamii, hivyo ni budi kuwaelimisha kwa kuandika habari zinazogusa haki za binadamu, ili waweze kufahamu haki zao,  wajibu wao na kuweza kuzisemea.

‘’Tunawaomba Wandishi muchukuwe jitihada za makusudi kuielimisha jamii kwa kuandika na kuripoti habari  zinazo husu haki za binadamu, ili waweze kuzifahamu na kuweza kuzitetea ,’’alisema.

Akiwasilisha mada juu ya haki za binadamu Mwanaharakati kutoka shirika la Msaada wa Kisheria  Pemba [ZALHO] Siti Habibu Mohd alisema miongoni mwa haki za msingi ambazo anatakiwa azipate binadamu ni kama vile Elimu, Kupiga kura, Matibabu pamoja na kumiliki mali.

Alisema endapo  wandishi watandika ipasavyo masuala ya haki za binadamu pale watakapona zinavunjwa kutapelekea  kuchukuliwa hatuwa na kuweza kutatuliwa kwa haraka.


Kwa upande wake Mratibu wa shirika la Maendeleo la Kimataifa Gamaliel Sun alisema bado jamii haina uwelewa juu ya masuala ya haki za binadamu, hivyo ni jukumu lenu wandishi wa habari kutumia taluma yenu kutoa elimu na kuona jamii wamepata ufahamu juu ya masuala hayo.


Mafunzo hayo ya siku Nne kwa wandishi wa habari yenye lengo la kuwahamasisha wandishi kuandika na kuripoti habari zinazo husu haki za binadamau yameandaliwa na shirika la mtandao wa asasi za kiraia Pemba [Pacso] chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa [UNDP].



  

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO