WANCHI WAHIMIZWA KULA VYAKULA VYENYE LISHE BORA
NA SALIM HAMAD, PEMBA
WANANCHI Visiwani
Zanzibar,wamehimizwa kuwa na uataratibu wa Unywaji wa maziwa ili
kujenga afya zao na kujikinga na magonjwa mbali mbali
yanayoweza kuwapata ikiwemo utapiamlo.
Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Halima Khamis Ali alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na
wananchi katika hafla ya unywaji wa Maziwa huko Maonesho ya Chakula Chamanangwe
Kisiwani Pemba.
Alisema Watu wengi hawana muamko wa unywaji wa maziwa jambo
linalodumaza afya hasa kwa watoto wadogo, hivyo ni wajibu wa kila mwana jamii
kutambua umuhimu wa suala hilo.
Alisema mbali ya kuwa jamii imehimizwa jambo hilo lakini
wanapaswa kufuata utaratibu unaotolewa na maafisa wa afya katika utumiaji wa
lishe hiyo.
‘’Kila mmoja kwa nafasi yake anawajibu wa kuihamasisha jamii
umuhimu wa unywaji wa Maziwa kwani yamekuwa yakisadia katika kujenga afya
zao huku yakiwa mazuri kwa wanafunzi kwani yanaongeza akili’’alisema.
Mapema Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba,Khamis Bilali Ali
alisema Wizara hiyo imekuwa ikihamasisha utumiaji wa lishebora hasa kwa mama
wajawazito ikiwemo utumiaji wa maziwa na kuwanyonyesha watoto wao kwa
kipindi cha miezi sita baada ya kujifungua kabla ya kuwalisha kitu
Chochote ispokuwa maziwa.
“ maziwa ya mama ndio chakula kizuri kwa watoto kwani kinajenga
mwili na akili” alisema Mdhamini huyo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani kwa
upande wa Tanzania (FAO )Lela Miraji alisema shirika hilo
litaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika kuboresha
mifumo ya upatikanaji wa Chakula Duniani.
Naye Mkurugenzi Maendeleo ya Mifugo Asha Zahran Mohamed alisema
uzalishaji wa maziwa kwa siku lita 25,019 huku akifafanua kuwa kwa mujibu
wa takwimu ya maotokeo ya Sensa iliyofanyika hivi karibuni ilionesha ni
asilimia ndogo wa Unywaji wa Maziwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Alisema katika uzalishaji wa Maziwa kuna changamoto kubwa
inayojitokeza kwa wafugaji juu ya malisho ya Wanyama kutokana na maeneo
madogo ya Ufugaji hapa Zanzibar .

Comments
Post a Comment