WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA VYAKULA VYENYE LISHE BORA
WANANCHI Visiwani
Zanzibar,wamehimizwa kuwa na uataratibu wa Unywaji wa maziwa ili
kujenga afya zao na kujikinga na magonjwa mbali mbali
yanayoweza kuwapata ikiwemo utapiamlo.
Afisa
Mdhamini Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Halima
Khamis Ali alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi katika hafla ya
unywaji wa Maziwa huko Maonesho ya Chakula Chamanangwe Kisiwani Pemba.
Alisema Watu
wengi hawana muamko wa unywaji wa maziwa jambo linalodumaza afya hasa kwa
watoto wadogo, hivyo ni wajibu wa kila mwana jamii kutambua umuhimu wa suala
hilo.
Alisema mbali ya
kuwa jamii imehimizwa jambo hilo lakini wanapaswa kufuata utaratibu unaotolewa
na maafisa wa afya katika utumiaji wa lishe hiyo.
‘’Kila mmoja kwa
nafasi yake anawajibu wa kuihamasisha jamii umuhimu wa unywaji wa Maziwa
kwani yamekuwa yakisadia katika kujenga afya zao huku yakiwa mazuri kwa
wanafunzi kwani yanaongeza akili’’alisema.
Mapema Afisa
Mdhamini Wizara ya Afya Pemba,Khamis Bilali Ali alisema Wizara hiyo imekuwa
ikihamasisha utumiaji wa lishebora hasa kwa mama wajawazito ikiwemo utumiaji wa
maziwa na kuwanyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miezi sita baada
ya kujifungua kabla ya kuwalisha kitu Chochote ispokuwa maziwa.
“ maziwa ya mama
ndio chakula kizuri kwa watoto kwani kinajenga mwili na akili” alisema Mdhamini
huyo.
Kwa upande wake
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani kwa upande wa Tanzania (FAO
)Lela Miraji alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika kuboresha mifumo ya upatikanaji
wa Chakula Duniani.
Naye Mkurugenzi
Maendeleo ya Mifugo Asha Zahran Mohamed alisema uzalishaji wa maziwa kwa
siku lita 25,019 huku akifafanua kuwa kwa mujibu wa takwimu ya maotokeo ya
Sensa iliyofanyika hivi karibuni ilionesha ni asilimia ndogo wa Unywaji wa
Maziwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Alisema katika
uzalishaji wa Maziwa kuna changamoto kubwa inayojitokeza kwa wafugaji juu ya
malisho ya Wanyama kutokana na maeneo madogo ya Ufugaji hapa Zanzibar .

Comments
Post a Comment