WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUONGEZA BEI YA MWANI.
WAKULIMA wa
kilimo cha Mwani kisiwani Pemba wameiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kuwangalia tena kwa jicho
la huruma, kwa kuongeza
bei ya mwani.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mkulima Raya
Salim Faki kutoka Mjini Kiyu amesema bei ya mwani ya kilo shilingi 1000 bado ni
ndogo, ukilinganisha na gharama wanazozitoa wakati wa kulima.
Alisema dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya awamu ya
Nane ni kuwaimarisha wakulima wa Mwani kichumi, hivyo ni wakati kuongeza bei
hadi shilingi 3000.
‘’Bei ya shilingi 1000 haikidhi haja, kwani
Tunanunua Kamba pamoja na taitai kwa gharama kubwa,hivyo tunaiomba Serikali
ituengezee bei, ifike angalau elfu 3000,’’ alisema.
Kwa upande
wake mkulima Salim Mbarouk Haji alisema bado wakulima wa mwani hawajanufadika na zao hilo,
kwani kilimo hicho kina changamoto nyingi.
‘’Kiukweli hasa tusifichane wanaonufaika na
zao la mwani ni makampuni yanayo nunua mwani na sio wakulima, wakulima wanaishia kunyanyasika tu,’’
alieleza.
Aidha
alisema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa vitendea kazi ikiwemo Boti
za kuchukulia mwani.
‘’Tunasikia
tu kama kuna boti za mkopo ila sisi hatujazipa, hivyo tunawaomba wahusika watufanyie
msada na sisi watupatie tunateseka,’’alieleza.
Alisema wanatarajia kuanzia June mwakani kiwanda hicho
kitanza uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mwani, hivyo wakulima watapata
fursa ya kuuza bidhaa hiyo kwa bei nzuri.
Alisema kiwanda hicho kitakua na uwezo wa kuchakata tani zaidi 30,000 za mwani kwa mwaka, hivyo kuendelea
kuvumilia.




Comments
Post a Comment