KATIBU MKUU AHIDI KUSHUSHA NEEMA KATIKA SEKTA YA ELIMU

NA FATMA HAMAD, PEMBA

KATIBU mkuu wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Khamis Abdala Said amesema wizara itahakikisha inaboresha mazingira rafiki kwa walimu, pamoja na kuwapatia haki zao stahiki, ili wawe na hamu ya kusomesha, na kuleta ufaulu mkubwa kwa wanafunzi.

Katibu huyo ameyasema hayo kwa niaba ya Warizi wa Elimu na mafunzo ya  amali  Zanzibar Lela Muhamed Mussa wakati akifungua Kongamano la walimu ikiwa ni shamra shamra ya kuelekea siku ya madhimisho ya walimu duniani, huko Chuo kikuu cha Taifa Suza kilichopo Mchanga mdogo wilaya ya Wete kisiwani Pemba.

Amesema ni haki ya kila mwalimu kuhakikisha anapata stahiki zake ambazo anatakiwa kuzipaga.

‘’Tutashirikiana bega kwa bega na chama cha walimu ili kuona changamoto zinazo wakwaza walimu zimeondoka,’’alisema.


Kwa upande wake  Naibu  katibu  mkuu  wa  chama  cha  Mapinduzi  CCM  Muhamed  Said  Dimwa ameiomba Serikali kuanzisha Tume ya Utumishi ya walimu , jambo ambalo litasaidia kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili  walimu Visiwani Zanzibar.

‘’Naishauri Serikali ifanye mchakato  wa kuwanzisha Tume hiyo kwa haraka iwezekanavyo, ili kuona walimu wananufaika na tume hiyo na kuondokana na changamoto zinazo wakabili,’’alieleza.

Alisema kuwepo kwa tume ya utumishi ya walimu ni jambo jema, kwani kutapunguza changamoto zinazowakwaza walimu pamoja na kuepusha mianya ya kuwepo kwa mishahara hewa.


Akisoma  Risala  Katibu wa Chama cha walimu Zanzibar  [ZATU]   Haji Juma Omar ameiomba Wiazara kurejesha nauli za walimu ambao wanaishi mbali  na maeneo yao ya kazi, ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi

Akitoa salamu kutoka wizara ya Elimu Afisa mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba  Muhamed Nassor  Salim alisema wizara imeajiri zaid ya walimu 1446 kisiwani Pemba, lakini bado matokeo ya kidatu cha Nne hayaridhishi katika mikowa yote miwili ya Pemba.

Hivyo amewataka walimu wakuu kusimamia vyema majukumu yao na kuhakikisha  wanafunzi wanafanya vizuri katika mitihani yao.

 




Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI