KAMISAA WA SENSA AWAPA DARADA VIONGOZI WA SERIKALI


NA FATMA HAMAD,PEMBA

KAMISAA  wa   Sensa  ya  watu  na  makazi   ya  mwaka  2022  Tanzania  Zanzibar  Balozi  Mohammed  Haji  Hamza amezitaka Tasisi za Serikali kuzitumia  Takwimu za Sensa katika kupanga mipango kazi ya  shughuli  zao za kimaendeleo.

Balozi huyo ameyasema hayo wakati akuzungumza na Viongozi na mafisa mbali mbali wa Serkali katika mkutano wa uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa huko Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema endapo watazitumia takwimu za Sensa ipasavyo kutawawezesha kuendesha vizuri mipango yao ya kimaendeleo, hivyo ni wakati kwa Tasisi kuzifahamu Takwimu hizo na kuzifanyia kazi.

‘’Ni vyema yinyi viongozi kuhakikisha mnazipata kwa usahihi takwimu za Sensa na kuzifanyia kazi katika tasisi zenu, ili ziweze kuwasaidia katika mipango yenu,’’alisema.

Samba mba na hilo aliwaomba viongozi hao kuzifikisha takwimu hizo katika jamii, ili nawao waweze kuzifahamu na kuzitumia katika kuendesha maisha yao.


Akifunga mkutano huo Mwenye kiti wa bodi ya Takwimu Balozi Amina Salum Ali alisema zipo baadhi ya Tasisi hawana utamaduni  wa kuzitumia takwimu  za Sensa ipasavyo katika kupanga mipango yao ya bajeti.

Nae mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amesema takwimu hizo zitawawezesha kujua changamoto zilizomo katika maeneo yao, huku akiahidi kutowa elimu kwa jamii ili nawao waweze kuzifahamu.



Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO