JAMII YATAKIWA KUWACHA TABIA YA KUWABAGUA WATU WENYE ULEMAVU
SALIM HAMAD,PEMBA
MKUU wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuwafungia ndani watu wenye
ulemavu kwani kufanya hivyo kunawakosesha haki zao za msingi ikiwemo ya
kielimu.
Mkuu huyo
wa Wilaya ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza na wananchi katika kilele
cha maadhimisho ya wiki ya VIZIWI Duniani yaliyofanyika katika kiwanja Cha Tennis Mjini Chake Chake, Kisiwani Pemba.
Alisema wapo
baadhi ya wana jamii na wananchi kwa ujumla
wamekuwa na tabia ya kuwaficha watu hao kwa madai ya kuona aibu bila ya
kutambua kuwa kufanya hivyo ni kuwadhalilisha na kuwakosesha haki za msingi
ambazo wanapaswa kuzipata kama watu wengine.
Aidha
alisema hafurahishwi na watu wenya tabia za kuwadhalilisha watu hao na kutoa
wito kwa jamii kuacha kuwadhalilisha watu hao na badala yake kuwafanyia mazuri
kama watu wengine ili wasijiskie kuwa wametwengwa katika Jamii kutokanana na hali zao.
Alisema
Serikali imekuwa akiwathamini watu hao kwa kutengeneza mazingira rafiki ambapo
kwa sasa imeshajenga Shule ya Elimu Mjumuishi Kisiwani Pemba,ili kuona watu wa
aina hiyo wanapata elimu iliyobora kama watu wengine ili waweze kujiendeleza kimaisha.
‘’Wapo
baadhi ya watu wemkuwa wakiwaficha watu
wenye ulemavu kwa kuwafungia ndani jambo
hilo linawadhalilisha, watu wanapaswa kutokuwaficha na wanapaswa kuwatoa ili waweze kupata haki zao za msingi kama watu
wengine’’alisema Mjaja.
Kwa upande
wake Mratibu wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba, Mashavu
Juma Mabrouk, alisema kufanyika kwa maadhimisho hayo yanajenga uwelewa kwa jamii katika kuwathamini
na kupambana katika kupatikana kwa haki za watu hao.
Akisoma
risala katika maadhimisho hayo Katibu wa Chama cha Viziwi Zanzibar(CHAVIZA) Abdalla
Alawi Abdalla, alisema watu wewnye ulemavu wamekuwa wakikabiliwa na Changamoto
kadhaa hasa wakati wanapokwenda kutafuta huduma katika taasisi za umma
kutokuwepo kwa mazingira rafiki.
Alisema
Changamoto nyengine ni kukosekana kwa wataalamu wa lugha za alama kwa baadhi ya
taasisi na kuishauri Serikali kuweka watalamu ili kurahisisha upatikanaji wa
huduma kwa urahisi.
Hata hivyo ameiomba
Serikali kuendelea Kuboresha miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu kwenye
Ofisi za Umma sambamba na kupatiwa mikopo na fursa za ajira ili kujiendeleza
kimaisha.
Naye Naibu
Katibu wa Jumuiya ya watu wenye Ulemavu
wa Ualbino Pemba, Mudathir Sharif Khatib ameiyomba Serikali kuchukua
hatua kali za Kisheria kwa wale wenye tabia za kuwadhalilisha watu wenye
ulemavu .
Siku ya
Viziwi duniani huadhimishwa kila
mwaka ifika Septemba 30 kwa upande wa Zanzibar
madhimisho hayo yalifanyika kisiwani Pemba,huku kaulimbiyu ya mwaka huu ni dunia
ambayo Viziwi popote walipo wanatumia lugha ya alama".


Comments
Post a Comment