Wizara, wadau wajadili muongozo wa jinsia, ukimwi Pemba
NA FATMA HAMAD, PEMBA
AFISA Mdhamini wazara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Pemba Hafidh Ali Mohamed, amesema michango ya
wadau mbali mbali katika ripoti ya awali ya mapitio ya muongozo wa jinsia na
ukimwi, itasaidia kupatikana kwa mpango sahihi, utakaozingatia usawa wa
kijinsia.
Afisa Mdhamini
huyo aliyasema hayo, ukumbi wa Samail Gombani, wakati akifungua mkutano wa
kupokea ripoti ya awali, ya mapitio ya uchambuzi wa muongozo wa jinsia na virusi
vya ukimwi, uliowakutanisha wadau mbali mbali, kisiwani Pemba.
Alisema
wizara, ikishirikiana na Tume ya Ukimwi Zanzibar pamoja na wadau wengine,
imekuwa ikiweka vipaumbele katika masuala mbali mbali yanayohusu afya ya Jamii.
Alieleza
kuwa, kwa hivyo maboresho hayo ya mwongozo huo, utakao zingatia mwitikio wa jinsia
na Virusi vya ukimwi, utasaidia makundi yote ndani ya jamii kufikiwa na huduma
stahiki.
‘’Kuna maradhi
tofauti, ambayo yamekuwa yakiibuka ndani jamii ikiwemo Ukimwi, hivyo ripoti hiyo
itasaidia kuweka mpango mkakati, ili kuhakikisha jamii inajikinga nayo, na watu
wakawa na afya njema,’’alieleza Mdhamini.
‘’Tulihakikisha
tunafanya mahojiano na watalamu mbali mbali, kama vile makundi malum, watu wa serikali,
kupata maoni yao, ili kuona tunapata mitazamo tofauti ya watu,’’alieleza.
Alieleza
kuwa, uwepo wa muongozo huo kutasaidia kujua ni kwa namna gani mipango mbali mbali ya nchi, yamezingatia usawa wa kijinsia, hasa
katika upatikanaji wa huduma za Virusi vya ukimwi na Ukimwi.
.jpg)

.jpg)

Comments
Post a Comment