Hatari wanazozipata wajawazito wanaojifungulia nyumbani
NA FATMA HAMAD, PEMBA
MIMBA yangu ya nne manusura niiage dunia.
Katika maisha zipo siku ambazo mtu huwa hawezi kuzisahau, iwe kwa jambo la kufurahisha au kusikitisha.
Kwa mama mmoja wa Micheweni ambaye amejaaliwa kupata watoto wanne, hawezi kuyasahau yaliyomkuta wakati akiwa na mimba yake ya pili.
Mwana mama huyu alinielezea kwa majonzi jinsi uamuzi wa kudharau ushauri wa kupata huduma za kliniki mapema na kujifungua kwa msaada wa wataalamu wa afya kulipohatarisha maisha yake.
Mama huyu aliyetaka jina lake libaki siri kati yake na mimi aliniambia…. Abadan hatasahu siku aliyopata uchungu wa uzazi na kujikuta bila ya kufahamu akiwa hospitali amewekewa chupa ya maji.
Alisema alijifungua mimba yake ya pili na kutokwa na damu nyingi hadi kupoteza fahamu.
Baada ya kujifungua hakupata fahamu mpaka alipozinduka na kukuta amewekewa chupa ya maji katika hospitali ya Micheweni, Kaskazini Pembaa.
Mume wa huyo mama alisema baada ya kuona hali ya mke wake ni mbaya alifanya haraka kukodi gari usiku na kumharakisha hospitali.
ndipo usiku huo alipokodi gari na kumpeleka Hospitali. Hali hi
ilimpelekeakutuimia pesa nyingi ili kunusuru maisha ya mkewe na mtoto na
kuiweka familia katika hali ya furaha.
‘’Nilipata funzo kubwa
na muhimu. Siku hizi nikiona mke wangu anazo dalili za uchungu wa uzazi
huwa namuharakisha hospitali kwa sabu huko ndiko unapopatikana
ufumbuzi uhakika wa matatizo na dawa zinazohitajaika kumtibu’’, alieleza
mme wake.
Miongoni mwa wanawake waliokutana na mitihani ya aiani hii ni Bibi Halima Juma wa Mjini Kiuyu, wilaya ya Wete, ambaye alipata misukosuko kutokana na kulea mimba zake tatu na kujifungulia nyumbani.
Alidai kuwa miongoni mwa mambo yaliyompeleka kutokwenda hospitali ni lugha za madaktari, nenda rudi isiyozaa matunda na hata suala la uhaba wa watalamu halimshawishi kujifungulia hospitali. .
Maryam Said mkaazi wa Chake chake ambae anaishi na virusi vya ukimwi kwa muda wa miaka 18 alimuambukiza mtoto wake wa mwanzo mambukizi ya virusi vya ukimwi.Kwani mimba yake ya kwanza, alijifungulia nyumbani, kwa hofu ya kwenda
Hospital kwa kuogopa kunyanyapaliwa.
‘’Hadi leo najilaumu, na najutia nafsiyangu, kwa kitendo cha kutokimbilia
hospitali kwa ajili ya kwenda kujifungua nikidhani kwamba nyumbani ni
salama,’’anasimulia.
Kwasasa ameshajifungua watoto wengine watatu, ambao wako salama na vvu,
baada ya kusikiliza na kutekeleza kwa vitendo ushauri wa watalamu wa afya.
Khadija
Khamis mama wa watoto watano,mkaazi wa Sizini hadi leo hii bado hajafikiwa na elimu
ya kuhudhuria kliniki na ndio maana hufika kwa watalamu baina ya miezi sita
hadi saba ya ujauzito wake.
‘’Mimi sipendi kwenda kituo cha afya ikiwa bado mimba ni changa, si pendi ile kila siku nenda na keshokutwa uje tena naona tabu,’’anfafanua.
MTAALAMU WA AFYA HUDUMA YA MAMA NA MTOTO
Akieleza
athari anazozipata mama mjazito anapojifungulia nyumbani Maryam Ali Said Mratibu
wa huduma za mama na mtoto Pemba anasema moja
ni kukosekana kwa huduma za mapema
za kimataibabu kwa mama mjamzito.
‘’Inawezekana ikawa mama hawezi kujifungua kwa
njia ya kawaida, analazimika afanyiwe upereshini, lakini mkunga wa jadi hana
taluma ya kujua hilo,’’anaeleza.
Anasisitiza kuwa kuhudhuria kituo cha afya kuanzia
wiki ya mwanzo ya ujauzito hadi kufikia kujifungua ni lazima kwa mjamzito ili
kujikinga na majanga.
‘’Kujifungulia
nyumbani ni sawa na kununua mauti, ya mama na mtoto wake, maana hakuna mtalamu,
vifa vya kinga ya maradhi na wengine wanaishi mbali na vituo vikuu vya
afya,’’anasema.
‘’Kama mama atakua ana mambukizi kama vile Homa ya Ini au Virusi vya ukimwi bila ya kutumia kifaa chochote, anaweza kusababisha mtoto, mkunga kupata mambukizi,’’ anaeleza.
Mjamzito anaejifungulia nyumbani, anaweza kupata
athari kiwemo kukaa kwa muda mrefu na uchungu, jambo ambalo linaweza
likapelekea kuchanika haraka kwa fuko lake la uzazi.
‘’Mara nyingi
wanapokuja Hospitali inakua mama ameshachoka, hali taabani, mpaka iwe
wameshashindwa, hata ukija ukitoa tena izo tiba muda umeshapita,’’ afafanua mtaalamu.
Alifahamisha
kuwa unapochanika kwa fuko la uzazi maranyingi mama hutokwa na damu nyingi
ambayo inaweza kusababisha hata kifo chake.
‘’Unapochanika
kwa fuko la uzazi, hatuwezi kusema kama ndo mwisho, lakini kama hukuwahiwa
mapema kupatiwa matibau unaweza ukapoteza maisha,’’anafafanua.
‘’Kuna siku tulimpokea mama na alikuwa ni ujauzito wake wa tatu,
alivyo kuja akapelekwa kwenye chumba cha kujifungulia, kabla ya kumlaza kwa
ajili ya kujifungua, tulimuhisi kalala kumbe ameshafariki,’’anasimulia.
Amina Omar
Msellem mkaazi wa Chake chake anasema amejifungua mimba saba na zote ni kituo
cha afya, wala hajapata changamoto yoyote yeye wala watoto wake.
Abdala Nassor
Abdala mwananchi wa Chake chake anasema
mama anapojifungulia nyumbani, mazingira
ya usafi Pamoja na usalama wa mama kujifungua salama yanakua
hayatoshelezi.
Mkewake
amejifungua mimba nane na zote alikua anampeleka Hospitali wakati anapoumwa tu
na uchungu,’’anafahamisha.
Mkuu wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja anasema ni vyema kwa wizara ya
Afya kuongeza mkakati wa elimu ili
wanawake washawishike kujifungulia hospitali.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui anasema
wizara imeimarisha miundombinu ya
kutolea huduma Hospitalini, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Afisa Mdhamin wizara ya Afya Khamis
Bilal Ali amewataka wahudumu wa afya kuwa na lugha nzuri kwa wajawazito ili iwe
ni sehemu ya ushawishi ya kuhudhuria kliniki.
‘’Wizara kwa upande wake inaendelea kuimarisha miundombinu bora ikiwemo
vifaa tiba dawa, lakini ni nafasi kwa watalamu wetu wa Afya nao kutumia lugha
laini ili kufanikisha hilo’’,anasema.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka ofisi ya mama na mtoto Pemba,inaonyesha kuwa
kwa mwaka 2022 mama 2019 walijifungulia
nyumbani, kati ya hao wane [4]
walifariki.
Waliojifungulia Hospital ni 16269 kati ya hao, Micheweni ni 985, Mkoani
754, Wete 9445 na Chake chake 5365, ambapo waliofariki kutoakana na uzazi ni
15.
Takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu, wajawazito
waliojifungulia nyumbani ni 1450, kwa upande wa wilaya ya Mkoani walikua ni 270, Chake chake 99, Micheweni 230 na Wete ni
292.
Ingawa wanaojifungulia Hospital kwa Pemba ni 8481, ambapo kwa wilaya ya Mkoani ni 1562, Chake chake 2601,
Wete 2140 na Micheweni 2178, huku vifo vikiwa tisa [9], ambapo Wete na
Micheweni kulikuwa na vifo vitatu vitatu.
SERA NA SHERIA.
Sera ya wizara ya Afya ya Zanzibar ya mwaka 1990 ni kuhakikisha inaimarisha huduma za afya ya uzazi ya mama na mtoto, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vya watoto wachanga.

.jpg)


Comments
Post a Comment