KUKIMBIA KWA WATUHUMIWA KUNACHANGIA KUONGEZEKA KWA UDHALILISHAJI

 

NA FATMA HAMAD, PEMBA

UKIMBIAJI wa watuhumiwa wa matukio ya udhalilishaji ni moja ya sababu inayokwamisha kesi za udhalilishaji zisiendelee na kushindwa kupata hatia.

Wakizungumza katika mkutano wa kuwasilisha ripoti za udhalilishaji za mwaka 2023,huko ofisi za Tamwa Chake chake, wanamtandao wa kupambana na udhalilishaji kisiwani Pemba wamesema jambo ambalo limeonekana ndio muaraubaini wa kumaliza kesi za udhalilishaji, ni kuwakimbiza watuhumiwa wa makosa hayo.

‘’Kesi zinakaa kwa muda merefu vituo vya Polisi ukiuliza unambiwa inafanyiwa uchunguzi, lakini ukiangalia huyo mtuhumiwa mwenyewe alishakimbia, sasa sjui anafanyiwa uchunguzi nani, kweli hivi tutafika wapi jamani,’’walisema.

Walieleza kuwa kuna mchezo maalumu umekuwa ukichezwa kwa makusudi wa kuwatorosha watuhumiwa,ili kesi zisiendelee katika vyombo vya kutolea haki.

Mapema mwanamtandao kutoka wilaya Wete Rashid Hassan Mshamata alisema kila mmoja kwa nafasi yake kuwa na umakini wa hali ya juu, kuepuka makosa madogo madogo, kuanzia vituo vya mkono kwa mkono hadi mahakamani, ili kukwepa mianya ya kutorosha na kuachiliwa huru kwa watuhumiwa.

 ‘’Kuna siku daktari alikosea kuandika tarehe tu, ya ile aliyo mhudumia muhanga, hapo wakili alipata njia na alin’gan’gania hapo hapo,’’alieleza Shamata.

Kwa upande wake mwanamtandao kutoka wilaya ya Mkoani Haji Shoka alieleza kuwa ili kuona kesi hizo zinamalizika na kupatikana kwa hatia ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake kuwacha rushwa muhali.

 ‘’Unaweza ukampeleka muhanga Hospitali ukambiwa ni mzima hajafanyiwa lolote,lakini ukimuangalia hata kukaa kitako hawezi, tunakwenda wapi, turudini kwa mwezi Mungu janai,’’ alieleza Haji Shoka.

Nae Afisa msimamizi wa mradi wa Tumia jukwaa la habari kumaliza vitendo vya udhalilishaji Zaina Abdala Salim aliwapongeza wanamtandao hao kwa juhudi waliozichukua dhidi ya mapambano hayo, huku akiwataka kuendelza juhudi zao hizo, ili kuona udhalilishaji imekua historia Zanzibar.

Kwa mwaka 2023 Jumla ya kesi 27 zimeripotiwa katika wila ya Mkoani, ambapo 18 zipo Polisi,1 imepata hukumu na fine, 1 fine, 3 zimeondolewa mahakamani kwa kukosa ushahidi, 4 zinaendelea Mahakam.

kwa upande wa wilaya ya Micheweni kuliripotiwa jumla ya kesi 21, ikiwa kesi 3 zilimalizika kwa kutolewa fain pamoja na fidia kwa sababu ilikua ni za watoto,7 zipo upelelezi na watuhumiwa tayari walishakimbia,4 zinaendelea mahakamani, 1 inasubiri kipimo cha DNA, 2 zilifungwa kwa amri ya Dpp, 1 iliachiwa huru kutokana na kukosa ushahidi, na 1 inasubiri tathmini ya ustawi.

Na Wilaya ya Wete kuliripotiwa kesi 45, ambapo 25 zipo upelelezi, 5 zipo DPP, 9 zinaendelea  Mahakamani, 2 zilipata hukumu,na 2 zilifutwa kwa kukosa ushahidi.




Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO