KITUO CHA AFYA CHA TAJWA NI CHANZO CHA WAJAWAZITO KUJIFUNGULIA MAJUMBANI

 

               NA FATMA HAMAD,

Wananchi wanaoishi kijiji cha Mjini Kuyu Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,  wavunja ukimya na kutoa kilio chao  kutokana  baada ya kuwekeza nguvu na pesa zao kwa  ajili ya kujenga kituo cha afya, lakini kimeshindwa kutumika na kutoa huduma kwa sababu ya kukosekana kwa wahudumu wa Afya .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Mwananchi  khamis  Omar  alieleza kuwa walifanya mchango nyumba hadi nyumba  wa vifaa vya ujenzi pamoja na kushiriki katika ujenzi na kujenga kituo cha afya, na   Serikali ikawasaidia  katika kuwezeka kituo hicho. 

 Hata hivyo, tokea mwaka 2011  mpaka sasa kituo  hicho  hakitumiki  na  kimekuwa  gofu.  

‘’Kituo hicho tulikijenga  kwa nguvu zetu na pesa zetu, na Serikali ikaja ikatusaidia kuezeka,  ila tunashangaa  Serikali  yenyewe  imekitelekeza, kipotu kinaporomoka, hakitumiki,’’alifahamisha  Khamis.

Alisema huu ni mwaka wa 12 tokea kujengwa kwa kituo hicho, ambapo kilifunguliwa  na  mbio za mwenge kwa shangwe na nderemo, ili kuondosha shida za wananchi wa kijiji hicho.

 Alisema baada ya kuona wanapata tabu kwa kufuata huduma za afya masafa marefu, ndipo wakamua wao wenyewe  kujitolea kujenga ili waondokana na kadhya hiyo, lakini  bado wanaendelea tu kuteseka.

‘’Tunaiomba Serikali itujali na ituonee huruma, ituwekee  kituo wananchi wake tunateketea,’’ alieleza mwananchi.

Mapema mwanachi  Raya  Hassan  Alisema kukosekana kwa kituo cha afya karibu na makaazi yao wanapata shida hususan wanapopata mgonjwa wakati wa usiku.

Alisema wanachukua  masafa  kilo mita nne kufuata huduma ya afya, ambapo  wanalazimika kupita sehemu za vichaka na mabonde.

 ‘’Hospitali ipo mbali, na hatuna daktari kijiji kizima hichi, hivyo tunapopata mgonjwa  au mzazi wa ghafla hususan nyakati  za usiku inashindikana   kupata  huduma  kwa haraka,  sisi  hatujui  tumfanye nini,’’ alisema bi Raya.

Bikame  Bakar Darusi   alisema  kuwa kukosekana kwa kituo cha afya kunachangia  kwa kiasi kikubwa  wa mama wajawazito   kujifungulia majumbani.

‘’ Mimi binafsi  mtoto wangu alitaka kujifungulia   njiani, kwani  barabara yenyewe hatuna, usafiri ni boda boda tu, gari za abiria hazifiki hususan kipindi cha mvua, hivyo wazazi wengi huishia kujifungulia njiani,’’ aliseleza kwa masikitiko   Bikame.

‘’Tunaiomba Serikali ituonee huruma tunapata shida hususan sisi wazazi, tunaomba hichi kituo mutuekee kitoe huduma japo za zarura, japo huduma za mama na mtoto tu,’’ alisema Bi Kame.

Alisema kuwa uzazi wa sikuhizi ni mashaka, hivyo ni vyema kituo kiweze kutoa huduma ili kulinda usalama wa mama na mtoto.

Diwani wa wadi  hiyo Bi Nasra  alisema yeye pamoja na sheha tayari wameshafuatilia kila sehemu ili kuona kituo hicho kinatoa huduma, lakini imeshindikana.

 ‘’Ijapokuwa kinajengwa kituo katika eneo la kiuyu minungwini, lakini ni vvyema kuwangaliwe tena kwa jicho la pili, kwa vile kijiji cha mjini kiuyu ni kijiji cha ndani, na  hakuna  hata miundombinu  ya  barabara,’’ alieleza diwani.

Afisa mdhamini wizara ya Jinsia  na maendeleo ya jamii Khamis Bilal Ali  alifahamisha kuwa wanajenga Hospitali  katika eneo la kiuyu minungwini ambayo itawanufaisha wananchi wa Minungwini pamoja na wa  mjini kuyu.

Alisema kuwa  jingo hilo walilolijenga watalitumia kukiwa na kesi maalumu kama vile mripuko wa maradhi pamoja na kipindi cha utoaji wa chanjo za watoto.




 



Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO