Jamii yatahadharishwa kuachwa nyuma wanawake wenye ulemavu mradi mabadiliko tabia nchi
Na Fatma Hamad- Pemba …...hana mguu, hana mkono, haoni, atawezaje kutunza mazingira……. HAYO NI MANENO ya ALi Juma Mbarouk kiongozi wa kamati ya uhifadhi mazingira Chwale anasema wanawake wenye ulemavu ni vigumu kuingizwa kwenye kamati za utunzaji mazingira. Anasema kamati yake, ina wajumbe 15, kati ya hao hamna hata mjumbe mmoja mwanamke mwenye ulemavu. Anasema hajamshirikisha mwanamke yeyote mwenye ulemavu, kwani anadhani hawezi kufanya shughuli hizo za uhifadhi kutokana na hali zao. ‘’Mtu aliekua hana mguu, hana mkono, wala haoni atawezaje kupambana na mabadiliko ya tabianchi hasa kwa kuwemo ndani ya kamati,’’anasema. VIONGOZI/WAJUMBE WA KAMATI Fatma Shaaban Mohamed ni kiongozi wa kamati ya kilimo mseto Shehia ya Mjini kiuyu, anasema katika kamati yake anao wajumbe 25 mtu mwenye ulemavu hana hata mmoja. Anasema hajawahi kum...