WANAOJISHUGHULISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA CHA MOTO KUKIONA
Na Is-haka Moh`d-Pemba Waziri waNchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Harusi Said Suleiman amewaomba Wazazi/Walezi Visiwani Zanzibar kufuatilia kwa karibu nyenendo za watoto wao ili kuwalinda kutumbukia katika janga la utumiaji wa dawa za kulevya. Waziri Harusi ametoa ombi hilo wakatia kifungua kongamano la siku ya maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya duniani ambapo kwahapa Zanzibar Kitaifa yameanzimishwa leo Juni 27 katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake Pemba. Alisema utumiaji wa dawa za kulevya umekuwa ukiathiri kwa kiasi kikubwa kwa vijana walio na umri kati ya miaka 9 na 45 ambapo vijana wengi huanza kutumia matumizi ya dawa za kulevya wakiwa katika Skuli za ...