Posts

UISLAMU NA UMILIKI WA ARDHI KWA MWANAMKE

Image
  Je, ni vipi uislamu unampa nafasi mwanamke kumiliki ardhi? NA FATMA HAMAD, PEMBA Kwa muda mrefu, kumekuwepo na dhana potofu katika baadhi ya jamii, hususan Zanzibar, kwamba mwanamke hana haki ya kumiliki ardhi. Dhana hii imejikita zaidi katika mila na tamaduni kuliko katika misingi ya dini ya Kiislamu. Viongozi wa dini na wanaharakati wa haki za wanawake wamekuwa mstari wa mbele kupinga mtazamo huo, wakisisitiza kuwa Uislamu unamtambua mwanamke kama mmiliki halali wa mali, ikiwemo ardhi. Ingawa viongozi wa dini ya kiislamu wanapinga mtazamo huo, wanaeleza kuwa mwanamke ana haki ya kurithi, kununua, na kutumia mali au ardhi kwa ridhaa yake mwenyewe. Kiongozi wa dini ya kiislamu kutoka kijiji cha Wingwi Njuguni kisiwani Pemba Juma Othman Nahoda  anasema ‘’Urithi ni haki ya mwanamke, na si hisani’’ Anasema katika Suratul- Nisa, aya ya saba (7) ‘’wanaume wanafungu katika walichoachiwa na wazazi wao na wanawake pia wanafungu katika walichoachiwa, iwe kidogo au kikubwa, ni fungu l...

Wanawake wenye ulemavu ambao waligombea na kukosa waomba kuangaliwa

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA WANAWAKE Wenye Ulemavu kisiwani Pemba ambao waliingia kwenye kinyan’ganyiro kugombea, katika   Uchaguzi mkuu 2025, wamemtaka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Ali Mwinyi kuwangalia kwa jichola huruma kwa kuwapa nafasi mbalimbali, ili walete mabadiliko kwa Taifa na kwa wenzao wenye Ulemavu. Akizungumza na mwandishi wa habari   hizi huko nyumbani kwao Katija Mbarouk Ali mwenye Ulemavu wa Viungo ambae aligombea Uwakilishi Jimbo la Kojani ingawa hakufanikiwa, alisema wamekua wakiingia kwenye kinyan’ganyiro ili kuona nawao wanaingia kwenye maamuzi. Alisema wakati kunapokuepo na nafasi za uteuzi kuwapa kipaombele wale ambao walijitokeza kugombea, ili kuwatia hamasa na moyo wa kuingia kwenye kinyan’ganyiro kwa wanawake hao wenye Ulemavu. ‘’Tumejitoa tumedharauliwa kwa sababbu tunapambana na watu wenye pesa na vyeo vyao, hivyo ipo haja Rais utuone, ili kufuta nguvu zetu ambazo tumezipoteza,’’alisema. Alisema watuWeny...

“Uchumi, unavyofifiza Ndoto za Wanawake Wenye Ulemavu kufikia uongoz’’

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA Katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2025, Tanzania imeshuhudia wimbi jipya la wanawake wenye ulemavu wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi  kutoka udiwani, ubunge hadi uwakilishi wa majimbo. Ingawa  nyuma ya safari hiyo ya kisiasa, kuna simulizi  ya kiuchumi, unavyosababisha  wanawake hao kufikia malengo yao ya kisiasa. Makala hii inachambua jinsi uchumi wa wanawake wenye ulemavu unavyoathiri ushiriki wao katika maamuzi, nafasi zao za uongozi, na sauti yao katika jamii ya Tanzania, hususan Zanzibar, kwa kuzingatia takwimu, sheria, na mikataba ya kimataifa. Utafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wa mwaka 2022, unaonesha zaidi ya asilimia 73 ya watu wenye ulemavu nchini, wanafanya kazi katika sekta zisizo rasmi hususan kilimo, uvuvi na biashara ndogondogo.  Maranyingi, wanawake wenye ulemavu wanabaki nyuma zaidi kwa sababu ya changamoto hiyo ya uchumi, mitaji na ukosefu wa fursa za kifedha, hali hii huwafanya kushindwa kugha...

MRADI WA SWIL ULIVYOLETA MABADILIKO KWA WANAWAKE WENYE ULEMAVU PEMBA

Image
  NA FAMA HAMAD, PEMBA Mradi wa kuwawezesha wanawake kudai haki zao za uongozi , demokrasia na siasa (SWIL)  umeandika historia mpya katika visiwa vya Zanzibar, umeleta nuru na matumaini kwa wanawake, hususan wale wenye ulemavu, waliokuwa kwa muda mrefu wakihisi kusahaulika katika safari ya maendeleo na uongozi. Mradi huo ulizinduliwa rasmi mwaka 2020 na unatarajiwa kumalizika Disemba 2026 umeonekana na mafaniko makubwa katika hatuwa mbalimbali za utekelezaji wake.   Utekelezaji huo wa (SWIL) ni ushirikiano kati ya  TAMWA-Zanzibar ,  ZAFELA ,  JUWAUZA , na PEGAO , umewafikia wanawake zaidi ya  4,000  katika wilaya za Pemba na Unguja, ukiwajengea uwezo, ujasiri, ari na ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Lengo kuu la mradi ni kuongeza ushiriki wa wanawake, ikiwa ni pamoja na wanawake wenye ulemavu, katika michakato ya uongozi, siasa na demokrasia Zanzibar (Unguja na Pemba) hivyo kuwawezesha kuwa “watendaji hai” badala ya kuwa ka...