Wasaidizi wa sheria wapewa mbinu
NA FATMA HAMAD- PEMBA Wasaidizi wa Sheria wametakiwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala ya udhalilishaji, ili kuona inaondokana na vitendo hivyo viovu ambavyo vimekua vikijitokeza siku hadi siku. Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wasaidizi wa sheria wa wilaya ya Micheweni Muhasibu wa Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Wilaya hiyo Riziki Ali Hamad juu ya masuala ya udhalilishaji, huko Tumbe wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema katika wilaya ya Micheweni bado kumekua kukijitokeza masuala ya ubakaji na ulawiti kwa watoto, hivyo ipohaja kwa wasaidizi wa sheria kuisaidia jamii kwa kuwaelimisha madhara yatokanayo na masuala hayo, ili kuona yameondoka. Akitaja sababu inayopelekea kujitokeza kwa masuala hayo ya ubakaji na ulawiti katika wilaya hiyo ni utelekezwaji uliokithiri wa wanawake na wato...