Posts

Showing posts from August, 2024

Wakulima waikumbusha jambo Serikali

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA Wananchi kisiwani Pemba ambao walikatiwa mikarafuu yao kwa ajili ya kupisha miundombinu ya umeme wameiomba Serikali ya Mapinduzi kuwalipa fidia zao wakulima hao. Wakizungumza katika hafla ya ugawaji wa zawadi kwa washindi wa Vuna na Tigo pesa mkulima Khamis Juma Khamis na Halima Mohamed Seif huko Makonyo Chake chake Pemba walisema walikatiwa mikarafuu yao na kuahidiwa kulipya ila hadi leo hakuna chochote walichokipata. Walisema kuwa karafuu ndio zao kuu wanalolitegemea kujipatia kipato, hivyo ni vyema Serikali kulikalia kitako na kuhakikisha wanalipatia ufumbuzi suala hilo. ‘’Tulikatiwa Mikarafuu yetu na tukaahidiwa tutalipwa ila hadi sasa hakuna lolote tulilolipata’’,walisema. Mapema mkulima Ali Kombo Hamad alisema katika msimu wa karafuu ujao ni vyema shirika la biashara la ZSTC kuboresha miundombinu ya kiwanda cha kununulia Makonyo kilichopo wawi, kuhakikisha kinafanya kazi ili kuwaondoshea usumbufu wananchi wanao kuja kuuza makonyo yao. ‘’Tulichuku...

TIGO ZANTEL wautunisha mfuko wa fidia kwa wanaoanguka mkarafuu

Image
                          NA FATMA HAMAD,PEMBA Mtandao wa simu wa Tigo Zantel umechangia shilingi milioni 350 kwenye mfuko wa fidia kwa ajili ya watu wanaopata ajali ya kuanguka mkarafuu wakati wakiwa katika harakati za uchumaji wa zao hilo. Akizungumza mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya milioni 350, huko Makonyo Chake ghake  Pemba, Mkurugenzi wa mtandao wa Simu wa Tigo Zantel Azizi Said Ali alisema wameamua kuchangia fedha hizo, ili kuuboresha mfuko huo ambao utawanufaisha wahanga. ‘’Kwa vile na sisi Tigo ni sehemu ya familia tumeamua kutoa mchango wetu ili kuona wanaopata ajali nawao wanaingizwa katika bima maalum,’’alisema. Akifungua hafla hiyo ya ugawaji wa zawadi kwa washindi wa vuna na Tigo pesa, Waziri wa biashara na Viwanda Zanzibar Omar Said Shaban amewataka wakulima wa zao hilo kuendelea kutumia mfumo wa malipo wa Tigo pesa katika kuuza karafuu zao. ‘’Niwaombe wananchi wenzangu endelea kuunga mkono m...

SIMU YAMPELEKEA KWENDA JELA MIAKA MINNE

Image
                                    NA FATMA HAMAD,PEMBA HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa   Wete Zuwena Mohamed Abdulkadir   amemuhukumu kwenda chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka minne     Ali Mbarouk   Suleiman mwenye   (18) mkaazi wa Konde Chanjaani   baada ya kutiwa hatiani kwa kuvunja Nymba usiku na kuiba   Simu. Mshitakiwa huyo ametiwa hatiani kwa makosa ya kuvunja nyumba na kuiba Simu moja aina ya Sumsung   yenye thamani ya shilingi 138,000/=, kwa makisio mali ya   Said Mohamed Salim . Aidha Hakimu huyo alieleza kuwa kosa la kwanza la kuvunja Nyumba usiku atatumikia   chuo cha mafunzo kwa muda wa mika mitatu, na kosa la pili la kuiba Simu atumikie kwa muda wa mwaka mmoja. Mbali na adhabu hiyo pia alitoa agizo la kurejeshwa simu kwa mwenyewe mmiliki wa simu hiyo ...

wanafunzi wametakiwa kujiepusha na vigenge viovu

Image
                         NA FATMA HAMAD,PEMBA Wanafunzi maskulini wametakiwa kujiepusha na vitendo hatarishi ambavyo vitasababishwa kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Micheweni (MIDIPAO)Hemed Said Masoud wakati akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya Tumbe Sekondari alisema kuwa wapo baadhi ya wanafunzi wamekua wakijingiza katika magenge maovu ikiwemo Ubakaji,wizi na ulevi. Alisema elimu ndio mkombozi mkubwa wa maisha, hivyo ni vyema wanafunzi kutumia muda wao kwa kujipatia elimu ambayo itakuja kuwaletea manufaa kwao na hata kwa familia zao. ‘’Niwausie wananfunzi wangu muda ukipita haurudi tena, hivyo itumieni fursa mlionayo kwa ajili ya kujipatia elimu bora ili isije ikawa majuto kwenu ya hapo badae,alisema mkurugenzi.’’  Mapema msaidizi wa Sheria shehiya Tumbe Magharibi Suleim...

Wizi wa Simu wamsababishia kwenda Jela miezi 6.

Image
                                      NA FATMA HAMAD,PEMBA Msifunzwa ni babae hufunzwa ni ulimwengu usemi huu umemkuta Sudi Hamad Salim mwenye umri wa mia 26 mkaazi wa Jadida Wete Pemba, kwenda Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi Sita baada ya kukubali kosa lake siku ya mwanzo ya kusomewa kesi yake. Awali mshtakiwa huyo akisomewa shauri lake   katika   Mahkama ya Wilaya iliyopo Wete   na Mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Juma Mussa Omar   alikiri kosa lake la kuiba Simu aina ya Tecno Spark   8 yenye thamani ya shilingi Laki 400,000 /=.   Mwendesha mashtaka huyo wa Serikali aliiambia Mahkama hiyo ya wilaya kwamba kwa vile mshtakiwa huyo amekiri kosa lake mwenyewe, ni vyema   kupewa adhabu kali ili iwe somo kwake na kwa wengine.   ‘’Mheshimi...