WANDISHI WA HABARI WAONESHWA NJIA
Wandishi wa habari wametakiwa kujikita zaidi Vijijini kuibua kero zinazo wakwaza Wananchi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud katika hafla ya madhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani huko Gombani Kisiwani Pemba.
Amesema wananchi wamekua wakikabiliwa na kero mbali mbali katika vijiji vyao, hivyo kama waandishi watawezakuziandikia zitaweza kutatua kwa haraka.
‘’Ndugu zangu wandishi wa habari msishie tu kuandika habari za Mkuu wa mkoa kasema, Mkuu wa wilaya kasema, nendeni vijijini mkaibue shida za Wananchi ili tupate kuzisikia na tuweze kuchukua hatua za kuzitatua’’alisema Mattar.
Aidha Mattar alisema uwandishi wa Habari unanafasi kubwa katika jamii kwa kuwafikiwa wasiokuwa na sauti hivyo amewataka waandishi hao kuelekeza nguvu zao katika kuandika Habari za Vijijini.
‘’Fani ya Uwandishi wa Habari ni sauti ya wasiokuwa na sauti shukeni Shukeni kwa wananchi kutafuta changamoto za Wananchi tupate kuzifahamu’’alisema Mattar.
Kwa upande wake Afisa mdhamini wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mfamau Lali Mfamau aliwasisitiza wandishi wa habari kufuata Miko na Madili ya kazi yao ili waweze kuandika habari zenye ukweli ambazo zitaleta tija kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.
Aidha mdhamini huyo alisema anasikitishwa na baadhi ya Viongozi wa Serikali kuwatumia watu ambao sio wandishi wa habari kufanya shughuli za kihabari, hali ambayo inakwenda kinyume na Sheria.



Comments
Post a Comment