WANDISHI WA HABARI WAPEWA SOMO
NA FATMA HAMAD,PEMBA Wandishi wa habari wametakiwa kuandika habari ambazo zitaihamasisha Jamii kulipa kipaumbele suala la michezo kwa wanawake ili kuona nawao wanashiriki katika mashindano mbali mbali Nchini. Wito huo umetolewa na Mkufunzi wa mafunzo ya masuala mbali mbali ya Jinsia na michezo Hawra Shamte wakati akizungumza na wandishi wa habari huko Ukumbi wa Tamwa Chake chak Pemba. Alisema bado Jamii hawampi kipaombele mwanamke kushiriki katika masuala ya michezo kutokana na dhana iliyojengeka kwamba mwanamke anaeingia kwenye michezo ni muhuni. ‘’Tumegundua kwamba Michezo yote ya wanawake imekufa kutokana na mfumo dume ambao umetawala katika Jamii ya Wazanzibar kwani wanasema michezo kwa mtoto wa kike ni uhun...