WATU WENYE ULEMAVU WAIOMBA SERIKALI KUONDOSHA VIKWAZO KWENYE MIKOPO.
NA FATMA HAMAD,PEMBA VIKUNDI vya Ushirika vya Watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba vimeiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwaondeshea vikwazo kwenye suala la upatikanaji wa Mikopo inayotolewa kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi kiuchumi ili kuona watu wenye ulemavu nawao wananufaika na fursa hiyo. Hayo yamesemwa na Omar Kombo Hamad kutoka kikundi cha Twamshukuru Allah kilichopo mbuzini na Fatma Salim Hamud wa kikundi cha Nia njema kutoka Ole kianga cha watu wenye ulemavu mara baada ya kumaliza mafunzo ya ya utengenezaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo Mafuta ya mgando ya mwani, mafuta ya mkaratusi pamoja na Jiki huko Ole mihogoni Chake chake Pemba. Walisema ili kuona watu wenye ulemavu wananufaika na fursa mbali mbali zilizomo kwenye Serikali, nivyema kupatiwa mkopo kwa mtu mmoja mmoja na isi...