UNYANYAPAA ADUI ASIEONEKANA KWA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU
NA FATMA HAMAD, PEMBA NI kawaida ya binadamu walio wengi wanapoumwa hunasibisha maradhi yao na imani za kishirikina. Na aina hii ya watu hawasikii, hawaoni wala hawashauriki kuhusu huduma za hospitali na hatimae kuangukia kwenye waganga wa kienyeji. Ingawa baadhi yao huelekeza imani zao kwengine baada ya kuona huduma za hospitali hazikuzaa matunda huku wakiwa wanaripoti kila wanapopangiwa. Ugonjwa wa kifua kikuu ni moja ya ugonjwa ambao watu wengi huelekeza imani zao kwengine kutokana na jinsi unavyokuja huku ukiwa dalili za mwanzo kutoonekana. ‘’Kila siku unapoenda hospitali ukisema unaumwa na kifua unapewa dawa tu bila kupimwa, hivyo hali ikiendelea kudhoofu mtu anajiona kama tayari ana magonjwa mengine ya kishirikina,’’ alisema mwananchi Faida Hassan mkaazi wa Finya Wilaya ya Wete, Anasema, wakati mwengine kutokufanyiwa vipimo ndipo kunakosababisha watu wengi kukimbilia kwa waganga wa kienyeji, jambo ambalo linaweza kuhatarish...