‘’Wandishi endeleeni kuipigia debe Sheria ya habari, ili irekebishwe’’
NA FATMA HAMAD, PEMBA Wandishi wa habari wametakiwa kuendelea kuipigia kelele Sheria ya habari, kuona imefanyiwa marekebesho na kuondoshwa vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari na vyombo vya habar. Alisema wandishi wa habari ndio wahanga wakubwa ambao wanaathirika kutokana na kuepo kwa Sheria inayominya uhuru wao kwani inapelekea kukosa baadhi ya tarifa. Akizungumza na wandishi wa habari katika mkutano wa tathmini wa mradi wa kudai uhuru wa habari, Afisa miradi na tathmini kutoka Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Mohd Khatib Mohd, alisema kukosekana na sheria rafiki hakuathiri wandishi wa habari pekeyao bali hata jamii kiujumla. Hivyo Afisa huyo alisema kuepo kwa hilo, ipohaja kuendelea kuandika habari zinazoshawishi kufanyiwa marekebisho na kupatikana kwa Sheria mpya Zanzibar. Mapema akiwasilisha ripoti ya mapitio a Sheria za Habari Afisa programu kutoka Tamwa, Zanzibar Zaina Abdalla Mzee, alisema licha ya juhudi mbalimb...