Posts

Showing posts from June, 2025

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

Image
                 NA FATMA HAMAD, PEMBA UTELEKEZAJI ni ile hali ya wazazi kukwepa majukumu yao ya kutoa matunzo kwa familia zao. Wengi wa wananchi wanadai kwamba, sababu kubwa inayopelekea utelekezaji ni baadhi ya akinababa wanapoamua kuoa mke zaidi ya mmoja, maranyi huwa hawatimizi wajibu wao. Ingawa wapo wengine, hudai kukumbwa na sababu, ya kutafuta maisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, mfano wa wavuvi au wafanyabiashara. Hayo yakifanyika, mafundisho ya dini yanafundisha kuwa, mzazi wa kiume ndio mwenye jukumu kubwa la kutoa matunzo kwa familia yake. Lakini ulimwengu wetu wa leo, kumeibuka wimbi kubwa la baadhi ya wanaume kukwepa majukumu  yao na kuwabebesha mzigo wa malezi wanawake peke yao. Hali hiyo ya wanaume kutokushughulikia familia zao, inasababisha watoto kuishi kwa simanzi na huzuni, kana kwamba wamefiwa na wazazi wao na kukosa familia ya kuwatunza. Kiongozi wa Kanisa Katoliki lililopo Mkungu Malofa Chakechake, Robert Mig...

Mfahamu Joahari, binti mwenye ndoto ya kua kiongozi

Image
                     NA FATMA HAMAD- PEMBA Kuwapa nafasi wasichana katika mijadala ya kisiasa, vikundi vya uongozi shuleni na vyuoni, , kunawajengea ujasiri wa kushiriki kwenye michakato ya kisiasa mapema na wakiwa na taarifa sahihi. Hili linasaidia kuvunja mila na desturi zinazoweza kuzuia wanawake kushiriki nafasi za uongozi  kwa   kiwango kikubwa. Kwa  kuanzisha  ushiriki  wao  mapema, tunaunda  kizazi  cha  wanawake wenye ujasiri na maarifa, ambao  watakuwa  tayari  kuwania  nafasi za  uongozi  na  kushiriki  kikamilifu  katika  kufanya maamuzi kwa maslahi ya jamii nzima. Hii pia inaongeza uwezekano wa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi wa kisera kuhusu masuala yanayohusu wanawake na vijana. Makala hii imezungumza na Johari Ibrahim Mbarouk ambae ni Rais wa Skuli ya Msingi Kiungoni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambae ana ndot...

‘’Wandishi wa Habari msiandike habari, zenye kuleta migongano’’

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid amewataka wandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli na zenye kuzingatia maadili, ambazo hazitosababisha uvunjifu wa amani Nchini. Mkuu huyo ameyasema hayo  wakati akifungua  Kongamano  la wadau wa Habari,  lililoandaliwa na Ofisi ya Rais Ikulu huko ukumbi wa ZRA Chakechake Pemba. Alisema vyombo vya Habari ndivyo ambavyo vinaweza vikaiweka Nchi katika hali ya Amani, ama kwenye migogoro, hivyo ni vyema wandishi mkatumia maadili yenu na kuandika habari zenye ukweli na zenye kuleta maendeleo,ili kuibakisha Nchi katika hali Utulivu. Alisema Serikali ya awamu ya nane imefanikiwa kuweka mambo mbalimbali ya maendeleo mjini na vijijini, hivyo ni jukumu lenu wandishi wa habari kuyandikia maendeleo hayo. ‘’Yapo mambo mengi ya maendeleo ambayo yamefanywa na Serikali yetu, hivyo yaandikeni hayo, ili yapate kufahamika, msiandike mambo ambayo yataleta uchochezi,’alieleza. Kwa upande wake Mkuu wa Wil...

Mjane wa watoto saba aomba msaada wa kuezekewa, ni baada ya kuachwa yeye na watoto wake

Image
                               NA FATMA HAMAD,PEMBA MJANE mwenye watoto saba amewaomba wahisani na watu wenye uwezo, kumpa msaada wa bati na miti, kwa ajili ya kuezekea nyumba yake, ili apate kustirika na watoto wake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kijiji cha Madenjani Wilaya ya Wete Pemba, mama Rehema Salum Issa ‘Vumilia’ alisema nyumba anayokaa imeshakua mbovu, mvua yote inamnyeshea ndani mwake. Alisema anapatashida kwani mvua inaponyesha husimama barazani hata kama ni usiku mkubwa,kwa vile ndani hujaa maji na kukosa sehemu salama. ‘’Ndani hujaa maji, vitanda vyangu vyote vimeshaharibika sina hata pakulala na watoto wangu saba, naomba binadamu wezangu munisaidie nateseka,’’alilalamika. Alieleza tayari alishajenga vyumba viwili vya matufali, ingawa ameshindwa kuezeka, hivyo ameomba asaidiwe bati pamoja na miti kwa ajili ya kuezekea, ili apate kuishi sehemu anapostahiki  binadamu. Alif...

Mdhamini Sheria ; ‘’Wasaidizi wa Sheria ifahamisheni jamii viashiria vinavyosababisha udhalilishaji’’.

Image
                     Na Fatma Hamad, Pemba AFISA MDHAMINI wizara ya Katiba Sheria na Utawala bora Halima Khamis Ali amewahimiza watoa msaada wa kisheria kuielimisha jamii, kufahamu mbinu za kuzuia vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, ambavyo vinaonekana kujitokeza siku hadi siku, ili waweze kujiepusha navyo Mdhamini huyo aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo watoa msaada wa kisheria juu kujikinga na vitendo vya udhalilishaji yaliofanyika ukumbi wa Katiba na Sheria Gombani Chakechake Pemba. Alisema vitendo vya udhalilisha bado vinaendelea kujitokeza na kuiathiri jamii, hivyo watoa msaada wanadhima kubwa ya kuwafahamisha wanajamii jinsi ya kujizuia na vitendo hivyo, ambavyo vimekua vikiwakosesha amani. ‘’Hata ukimshauri, ukimuelimisha aliepata hayo matatizo basi kunahitaji utaalamu, hivyo basi tuendeleeni kuisaidia jamii yetu ili kupata kizazi kilichosalama,’’alisema.  Aidha aliwasisitiza wato...