DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO
NA FATMA HAMAD – PEMBA SHAHIDI BASHE MAKAME Khamis ambae ni Afisa kutoka Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali Zanzibar ameiambia Mahkama ya Mkoa iliyopo Wete Kaskazi Pemba, k baada ya kufanya uchunguzi wa vinasaba katika Mashine ya DNA vipimo vimengudua kwamba mtuhumiwa Bahati Mashauri ndie baba mzazi wa mtoto aliezaliwa na binti aliembaka. Akitoa ushahidi wake mbele ya Mahkama hiyo ya Mkoa Bashe alidai kuwa baada ya kupokea vinasaba vya mtoto aliezaliwa na vya mtuhumiwa pamoja na mama aliezaa baada ya kubakwa, alianza kufanya uchunguzi wa vinasaba vya mtoto na mtuhumiwa na kugudua kwamba mtuhumiwa ndie baba mzazi wa mtoto kwa asilimia 9.99 Aidha alidai kuwa aliendelea kufanya vipimo vya vinasaba vya mtoto na mama yake pia aligundua kwamba mtoto ndie mama yake mzazi binti ambae...