Jumuiya za vyama vya siasa, muarubaini wa kuwasaidia wanawake kwenye uongozi
NA FATMA HAMAD, PEMBA MWENYEKITI wa CUF Mhamed Haji Kombo, wa Chake chake akiri kuwa uanzishwaji wa jumuia za wanawake ndani ya vyama vya siasa, zimesaidia kwani zimewaamsha wanaume kufahamu kwamba, haki ya kugombea ni kwa wanachama wote. Aanasema jumuia za wanawake zimezaa matunda kwani wanawake katika Chama chao wamekua na uthubutu wa kugombea nafasi za ungozi, ambapo ngazi za kitaifa viongozi wengi ni wanawake. ’ ‘Wamekuwa wakipata elimu na mafunzo mbali mbali kwenye jumuia zao, na ndo maana wakawa na uthubutu huo wa kuhodhi nafasi za uongozi,’’ Amesema Mohamed wakati wa mahojiano. Mwenyekiti wa Chama cha ACT WAZALENDO Mkoa wa Kusini Pemba kichama, Saleh Nassor Juma anasema mchango wa Ngome za Wanawake ni mkubwa kwani zimewafanya wanawake waondokanae na hofu ya kugombea na kushika nyadhifa za uongozi. ‘’Kwa kweli hizi Jumuia za wanawake kwenye vyaama zimewatoa hofu wanawake, maana ukiangalia kwenye kamati yetu ya uongozi ya Mkoa Cha...