WANAHARAKATI WAPAZA SAUTI KUTAKA UWEPOSUALA LA USAWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI

 


                               NA MADINA ISSA, UNGUJA

UTEKELEZAJI WA MIKATABA NA MATAMKO MBALIMBALI YA KIKANDA, KITAIFA NA KIMATAIFA JUU YA SUALA LA USAWA WA KIJINSIA BADO NI KITENDAWILI WISIWANI ZANZIBARKWANI WANAWAKE AMBAO NDIO WENGI NCHINI  KWA ASILIMIA 52   HAWASHIRIKISHWI IPASAVYO KATIKA NGAZI ZA MAAMUZI 

KWA MUJIBU YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MWAKA 2024 KWA ZANZIBAR IDADI YA MADIWANI WANAWAKE NI ASILIMIA 23, WAWAKILISHI ASILIMIA 16 NA KWA UPANDE WA WABUNGE NI WA 4 KATI YA 50 AMBAYO NI SAWA NA ASILIMIA 8

BI ZAWADI AMOUR NASSOR MWAKILISHI WA JIMBO LA KONDE   AMESEMA KWAKE HAIKUWA RAHISI KUPATA NAFASI HIYO KWANI WANAWAKE WANAPITIA CHANGAMOTO NYINGI KUFIKIA NDOTO ZA KUWA VIONGOZI IKIWEMO KUTOUNGWA MKONO NA JAMII INAYOWAZUNGUKA, KUVUNJWA MOYO PAMOJA NA UHABA WA FEDHA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI.

 AIDHA AMESEMA SABABU NYENGINE NI HOFU NA KUTOKUJIAMINI HALI INAYOPELEKEA WANAWAKE WENGI KURUDI NYUMA KUINGIA KWENYE KINYANG’ANYIRO CHA KUGOMBEA NGAZI MBALIBALI ZA KUWA VIONGOZI

HIVYO AMETOA WITO KWA WANAWAKE KUJITOA KUPAMBANIA NDOTO ZA KUWA VIONGOZI ILI WANAWAKE WENGINE NA WATOTO WAPATE WA KUWASEMEA KWA VILE WANAKABILIWA NA MAMBO MENGI AMBAYO YANAHITAJI SAUTI YA PAMOJA ILI KUTATULIWA KWA  HARAKA

MRATIBU WA MRADI WA KUINUA WANAWAKE KWENYE UONGOZI (SWIL) MARYAM AME CHUM AMESEMA KATIKA KUHAKIKISHA  USAWA UNAPATIKANA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE TAMWA ZANZIBAR KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE ZANZIBAR ZAFELA NA  PEGAO  WAMEWAPATIA UWEZO  WANAWAKE UNGUJA NA PEMBA HIVYO ANAIMANI YATAZAA MATUNDA KWA WANAWAKE KUGOMBEA KUANZIA NGAZI ZA CHINI HADI KWENYE   UCHAGUZI UJAO WA MWAKA 2024

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.