MKUGENZI WA CHAMA CHA WANDISHI WA HABARI WANAWAKE ATAKA KUWEPO NA USAWA WA KIJINSIA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI

 

                         NA MADINA ISSA,UNGUJA

MKURUGEZI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE TANZANIA TAMWA ZANZIBAR  DK MZURI ISSA  AMESEMA IKIWA ZANZIBAR IMO NDANI YA TANZANIA INAWAJIBU KUTEKELEZA MAKUBALIANO YA KIMATAIFA YA KUWEPO USAWA WA KIJINSIA KWENYE NAFASI ZOTE ZA UONGOZI

AKIZUNGUMZA NA KATI FM HUKO OFISINI KWAKWE TUNGUU MKOA WA KUSINI UNGUJA AMESEMA LICHA YA SHERIA NA  MATAMKO MBALIMBALI  BADO HALI YA UTEKELEZAJI WA SERA NA SHERIA HIZO HAURIDHISHI  NA NI KINYUME NA ILIVYORIDHIWA MIKATABA YA KIMATAIFA  KWANI TAKWIMU ZA NAFASI YA MWANAMKE UONGOZI WA USHEHA KWA ZANZIBAR NZIMA  UNGUJA NA PEMBA  NI  ASILIMIA 20 TU

AMESEMA UTAFITI UNAONESHA KUWA VIONGOZI WANAWAKE WANAFANYA KAZI VIZURI ZAIDI PINDI WAKIPATIWA NAFASI HIVYO NI VYEMA WANAOHUSIKA KATIKA UTEUZI WA NAFASI ZA USHEHA KUANGALIA WANAWAKE WANAOWEZA KUONGOZA NA UPATIKANE USAWA WA KIJINSIA KWA WOTE

KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI IDARA YA URATIBU TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA ZANZIBAR BI ZAINAB KHAMIS KIBWANA AMEKIRI UWEPO WA IDADI NDOGO YA SHEHA  WANAWAKE  NA KUSEMA KUWA INATOKANA NA SABABU MBALIMBALI  HUKU AKIELEZA KUWA WANAJITAHIDI KUHAKIKISHA  IDADI HIYO INAONGEZEKA SIKU HADI SIKU KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA.

KWA MUJIBU WA SENSA YA MWAKA 2022 IDADI YA WATU ZANZIBAR JUMLA NI 1,889,773. WANAUME WAKIWA 915,492 SAWA NA 48% NA WANAWAKE 974,281.  SAWA NA 52 % HUKU NAFASI YA UONGOZI WA USHEHA  WANAUME NI 80 %  NA WANAWAKE NI 20 %

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.