MASHEHA WATAKIWA KUWACHUKULIA HATUA WANAOVURUGA AMANI NCHINI

 

NA FATMA HAMAD, PEMBA

Mwenyekiti wa kamati ya madili Zanzibar Abdala Mnubi Abasi amewataka Masheha kushirikiana na kamati hiyo kuondosha vitendo viovu vinavyofanywa na watu wasio kuwa na khofu ya Mungu katika jamii zao, ili kulinda amani na silka za kizanzibar.

Mwenye kiti huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na Masheha wa wilaya ya Wete huko ofisi ya mkuu wa Wilaya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema katika  Ramadhani ya mwakajana waligundua jumla ya vituo 14 ambavo vilikua vinapikwa mchana wa mwezi mtukufu wa ramadhani kisiwani Pemba.

‘’Hata kama mtu si muislamu lakini hatakiwi kupika na kula mchana hadharani, hivyo niwaombe Masheha kuchukuwa hatua watu ambao wanakula kinyume na taratibu zilizowekwa na Serikali,alisema.

Aidha alisema katika mji wa Wete kuna vibanda ambavyo vinatumiwa na Mama ntilie kwa ajili ya kuuzia biashara zao, lakini ikifika nyakati za usiku vibanda hivyo hutumika kama ni sehemu za starehe, hivyo aliwataka masheha kuweka ulinzi shirikishi katika maeneo hayo ili kuthibiti vitendo hivyo viovu ambavyo vimekuwa vikifanyika siku hadi siku.

 Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuia ya Ukuwem kisiwani Pemba Yussuf Ali Said amesema vitendo vya mmongonyoko wa madili vimekithiri  katika maeneo yetu, hivyo ni wakati masheha  kuzitumia vyema nafasi walizonazo ili kuona wanasimamia vyema madili na kuhakikisha kunakuepo na kizazi chenye tabia njema.

‘’Ndugu zangu masheha nyinyi ni viongozi hivyo mtakwenda kuulizwa kesho mbele ya mungu juu ya ulivyoitumia nafasi yako katika kuwaongoza watu,alieleza.

Alieleza kuwa Kunawimbi kubwa la watu wanaokuja kuishi chini kwetu kutoka kisiwa cha Tanga na Tanzania bara, tunapowakodisha majumba yetu wamekuwa wakiyafanya madanguro, na ukiangalia wanaowatumia ni watoto wazaliwa wa kisiwani humu, hivyo ni budi kazitumia nafasi walizo nazo kuliangalia hilo, ili kunusuru vijana na vitendo viovu wanavyofanyiwa.

Nao baadhi ya masheha waliohudhuria mkutano akiwemo akiwemo Asha Khamis Sheha wa shehia ya Piki na Othman Ali Khamis walisema bado jamii haijakuwa tayari kusimamia vyema suala la madili kwa watoto wao.

‘’Mimi binafsi nilishawahi kupigwa na kesi imeenda Polisi kwa sababu nilikwenda  kuvunja ngoma ambayo ilikua inapigwa usiku mkubwa ambapo niliamini haina usalama ngoma hiyo nilipigwa na kesi ikaenda hadi mahakamani, alisema Sheha wa Mtabwe kusini.

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.