VIJANA WATAKIWA KUJIWEKEZA ZAID KWENYE MICHEZO
NA FATMA HAMAD, PEMBA
Vijana wamehimizwa kujikita zaidi katika suala la michezo hasa mpira wa miguu ambao umekuwa na mchango mkubwa wa ajira.
Hayo yamesemwa na Mkaguzi wa Ulinzi shirikishi kutoka shehia ya Pandani na Mlindo Khalfan Ali Ussi mara baada ya kumalizika kwa Fainali ya mpira wa miguu kati ya kikundi cha ulinzi shirikishi cha kijiji cha Masipa na Miburani, huko uwanja wa Pandani wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema mpira ni moja ya sehemu ya kujipatia ajira, hivyo wakati umefika kwa vijana kujiunga na mpira wa miguu, jambo ambalo litawawezesha kujipatia fursa zilizomo kwenye michezo.
‘’Mpira sasahivi umekuwa ni biashara kubwa Duniani, hivyo acheni kukaa tu kwenye vigenge kwa kisingizio kwamba hamna kazi ya kufanya, alisema.
Alieleza endapo Vijana watajishughulisha na michezo wataepukana na matendo maovu ikiwemo Ubakaji,Ujambazi na Wizi.
Alisema lengo la mashindano hayo ni kuwa weka pamoja na kuwashajihisha vijanahao kujiunga pamoja na kupanga mikakati zaidi ya kupambana na changamoto zilizomo katika Shehia zao.
Nao Vijana hao walimuahidi mkaguzi huyo kwamba wataendelea kuwasimamia na kuwapa Elimu wale ambao hawajakuwatayari kuacha vitendo vya kihalifu ili kuhakikisha wanaishi kwa Amani Vijijini mwao.
Kwa upande wao badhi ya wazazi waliohudhuria mchezo huo walimpongeza mkaguzi huyo, huku wakimtaka aendelee kuwa karibu na Vijana hao na kuwapa elimu juu ya kujitambua, ili wasijingize katika makundi maovu, na kuona wanakuwa watoto wenye madili mema.
Katika mtanange huo Masipa ilibuka na ushindi Penalti Nne kwa Tatu zidi ya Miburani.
.
.
Comments
Post a Comment