Posts

Showing posts from May, 2025

MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI ZANZIBA KUFANYIKA MEI 17

Image
                                                                                      Na Fatma Hamad- Pemba Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) imesema Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani yanategemewa kufanyika Jumamosi tarehe 17 Mei, 2025 katika ukumbi wa RAHALEO STUDIO kuanzia saa 2:30 asubuhi ambapo yatahudhuriwa na waandishi wa habari, wadau mbali mbali wa habari pamoja na wawakilishi kutoka taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali. Makamo mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Mzuri Issa amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yana ujumbe muhimu na adhimu ambao ni “Sheria nzuri ya Habari ni chachu ya uchaguzi ulio huru na wa haki” Maadhimisho hayo ni muhimu katika kukuza na kuimarisha kada ya habari hapa nchini pamoja na kutoa wito maalum kwa...

Ndoto ya kupata Sheria Mpya ya Habari Zanzibar mwaka huu yazimika

Image
                                 Na Fatma Hamad, Pemba SIKU ya Uhuru wa Habari Duniani ni siku inayotambuliwa ulimwenguni kote kwa sababu ya umuhimu wake. Kwa kuwa uhuru wa Habari ni haki ya msingi kwa binadamu wote na ndioyo maana Umoja wa Mataifa ukaitangaza Mei 3 ya kila mwaka kuwa ni siku ya Uhuru wa Habari. Kwa watetezi wa haki za binadamu. Wanahabari na wadau wa habari huiadhimisha siku hii katika mwezi mzima wa Mei kwa kutafakari, kujadili na kutathmini uhuru wa habari ulivyo katika eneo husika. Kama ilivyo kwa mataifa mengine waandishi wa habari Tanzania Zanzibar huadhimisha siku hiyo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali katika kutathmini na kuchochea uwapo wa uhuru wa habari nchini. Makala hii iliyoandaliwa na waandishi wa habari Kisiwani Pemba imebeba dhima ya kufanya uchechemuzi ili kupata Sheria Mpya ya Habari ya Zanzibar ili uhuru wa habari ulindwe na utekelezwe kama unavyoainishw...

WANASIASA WANAOGOPA KUTUMIA UHURU WA KUJIELEZA

Image
                       NA FATMA HAMAD-PEMBA Kila Raia ana haki ya kutoa maoni na kuwa na uhuru wa kujieleza Kifungu cha 18 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinaeleza kuwa ‘’Bila ya kuathiri Sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni na mawasiliano yake bila kuingiliwa kati.” Na hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 42 inaeleza kwamba, kila mtu anastahili kuwa huru bila kuathiri sheria za nchi. Kwa Zanzibar viongozi wa vyama vya siasa wanasema, wamekua wakikosa kutumia uhuru wao wa kujieleza, licha ya kuwa ni haki yao kikatiba. Hivyo basi, makala hii imezungumza na wadau mbali mbali pamoja na wanasiasa  ili kufahamu ni kwa nini wanasiasa wanaogopa kutumia uhuru wao wa kujieleza. WANASIASA Maryam Nassor Juma ambae ni Katibu wa Chama cha Chauma mkaazi wa Vitongoji Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba anasema, wanaogopa kutumia uhuru wao wa kujieleza kutokana na mifumo pa...

Wandishi ibueni kero zinazowakwaza wanawake, kushindwa kutimiza ndoto zao za kua viongozi

Image
  Na Fatma Hamad-Pemba CHAMA cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar kimewataka waandishi kisiwani Pemba kushirikiana  pamoja na  wahamasishaji jamii ( CBEES ) juu ya maswala ya wanawake na uongozi ili  kuongeza nguvu na kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake   na kuongeza ushiriki wao katika nafasi za uongozi. Wandishi wa Habari wametakiwa kujikita Vijijini, ili waweze kuibua kero zinazowakwaza wanawake, ambazo zinawafanya washindwe kugombea nafasi mbalimbali katika uongozi. Akizungumza na waandishi hao kutoka vyombo mbali mbali kisiwani Pemba Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka  (TAMWA) Mohamed Khatib Mohamed  waliofika katika mkutano maalum uliowakutanisha wahamasishaji jamii pamoja na waandishi hao uliofanyika katika ukumbi wa PEGAO Msingini Chake chake Amesema  katika miaka ya nyuma wanawake  walikua wako nyuma kushika nafasi za uongozi, kutokana changamoto mbalimba...