“Uchumi, unavyofifiza Ndoto za Wanawake Wenye Ulemavu kufikia uongoz’’
NA FATMA HAMAD, PEMBA Katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2025, Tanzania imeshuhudia wimbi jipya la wanawake wenye ulemavu wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi kutoka udiwani, ubunge hadi uwakilishi wa majimbo. Ingawa nyuma ya safari hiyo ya kisiasa, kuna simulizi ya kiuchumi, unavyosababisha wanawake hao kufikia malengo yao ya kisiasa. Makala hii inachambua jinsi uchumi wa wanawake wenye ulemavu unavyoathiri ushiriki wao katika maamuzi, nafasi zao za uongozi, na sauti yao katika jamii ya Tanzania, hususan Zanzibar, kwa kuzingatia takwimu, sheria, na mikataba ya kimataifa. Utafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wa mwaka 2022, unaonesha zaidi ya asilimia 73 ya watu wenye ulemavu nchini, wanafanya kazi katika sekta zisizo rasmi hususan kilimo, uvuvi na biashara ndogondogo. Maranyingi, wanawake wenye ulemavu wanabaki nyuma zaidi kwa sababu ya changamoto hiyo ya uchimi, mitajina ukosefu wa fursa za kifedha, hali hii huwafanya kushindwa kughar...