WAFANYA KAZI NCHINI WATAKIWA KUYATHAMINI MAPINDUZI YA ZANZIBAR

 

NA FATMA HAMAD, PEMBA

VYAMA  vya wafanyakazi Nchini vimetakiwa kuyalinda na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kwani ndio mkombozi mkubwa kwao.

Akizungumza na mwandishi  wa habari hizi Amina Omar Mselem kutoka Chama cha  Hudma Serikalini  na Afya [ZUTI] amesema vyama vya wafanya kazi ni miongoni mwa vyombo vilivyosaidia kupambana hadi kuhakikisha Serikali imepata uhuru wake.

Alisema Mapinduzi yameleta faida  kwa watu wote, hivyo ni vyema kulindwa na kuthaminiwa, kwani yameondosha Ubaguzi katika mambo mbali mbali Nchini.

Alisema kuwepo kwa mapinduzi ya Zanzibar kumewakomboa Wanawake, katika Nyanja Mbali mbali ikiwemo Kiuchimi Kisiasa jambo ambalo limefnya mwanamke kuwa na uthubutu wa kuweza kushika nafasi mbali mbali za uongozi.

‘’Tunawashukuru Viongozi wetu wapendwa waliofanya juhudi nakutukomboa, kwani wanawake ilikuwa kazi yetu ni kufanyishwa kazi hatukuwa na uhuru,alisema.

Alieleza kwa sasa wanawake wamekuwa na uhuru wa kuzungumza popote na kusikilizwa maoni yao na kufanyiwa kazi.

 Aidha aliendelea kusema wamefarajika kuepo kwa Mapinduzi kwani Matibabu Hospitalini yanapatikana bure wakati wowote muda wowote unapohitaji.

 Shaame Suleiman Shame mwananchi kutoka Kijiji cha Sizini alisema miongoni mwa faida za Mapinduzi ni kuwepo kwa Elimu bure, ambayo inapatikana na kwa kila mtoto ambae ameshafikia umri wa kusoma.

‘’Kabla ya Mapinduzi waliokua na haki ya kusoma ilikuwa ni watoto wa Viongozi tu, na sisi watoto wa wakulima ilikuwa ni ngumu kupata Elimu, alieleza.

Naye Mbarouk Hamad kutoka Tumbe alieleza kuwa Mapinduzi yamekuwa ni mkombozi mkubwa kwao, kwani zamani ilikuwa wa Afrika kupata ajira ya Serikali ni mwiko.

‘’Tunashukuru sasahivi hakuna ubaguzi uwe moto wa Kiongozi, masikini unajiriwa alimradi uwe umetimiza vigezo na masharti ya ajira’’alisema Mbarouk.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.