WIZARA YA AFYA WATOA USHAURI KWA WANDISHI WA HABARI
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Wandishi wa
habari wamehimizwa kuendelea kuielimisha
jamii kufahamu umuhimu
wa chanjo ili waweze kujitokeza kwa wingi vituo vya afya kupata
chanjo jambo ambalo litawaepusha na maradhi mbali mbali ikiwemo shurua, Saratani ya shingo ya kizazi pamoja na
Korona.
Wito huo
umetolewa na Afisa mdhamini wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali katika
mkutano wa tathmini ya huduma wa mpango
wa chanjo zinazotolewa Zanziba ya
mwaka 2022 kwa
wandishi wa habari
huko baraza la
mji Chake chake
Pemba.
Amesema
jukumu kubwa la wandishi wa habari ni kuielimisha jamii katika masuala mbali
mbali ya kimaendeleo, hivyo ni wakati
kwa wandishi wa habari kuwafahamisha wananchi kupata chanjo zinazotolewa
na wizara ya Afya kwa usahihi ili kuepusha vifo vya watoto na jamii kiujumla.
‘’Ndugu
zangu wandishi wa habari tunawaomba mtusaidie kuifahamisha jamii wawapeleke
watoto wao wapate chanjo ili kuwakinga na magonjwa hatarishi’’ alieleza afisa
mdhamini.
Aidha
amefahamisha kuwa licha ya kiwango cha chanjo kuwepo juu lakini bado kuna
tatizo la mabinti wengi walio katika
umri wa miaka 14 hawapati chanjo ambazo zitawakinga
na maradhi tofauti ikiwemo saratani ya
shingo ya kizazi kutokana na uwelewa mdogo uliopo katika jamii kwa.
Mapema mkuu
wa kitengo cha chanjo ofisi ya Pemba
Bakar Hamad amesema kuwa chanjo zote zinazotolewa na wizara ya afya ziko salama
hazina madhara yoyote, hivyo wazazi wawachomeshe watoto wao bila ya woga
wowote.
Amesema kwa
mwaka huu wa 2023 wizara imejipanga kutoa huduma ya chanjo
hadi maskulini ili kuhakikisha watoto wote na wasichana wamepatiwa chanjo hizo.
Nae mkuu wa
kitengo cha huduma za Chanjo Zanzibar Abdul hamid Ameir Saleh amewataka
wandishi wa habari kushirikiana na kitengo cha chanjo na kurusha habari zinazo husu kitengo hicho ili wananchi
waweze kuchukua hatua ya
kujikinga dhidi ya maradhi hatarishi.
Comments
Post a Comment