Posts

MASHEHA WATAKIWA KUWACHUKULIA HATUA WANAOVURUGA AMANI NCHINI

  NA FATMA HAMAD, PEMBA Mwenyekiti wa kamati ya madili Zanzibar Abdala Mnubi Abasi amewataka Masheha kushirikiana na kamati hiyo kuondosha vitendo viovu vinavyofanywa na watu wasio kuwa na khofu ya Mungu katika jamii zao, ili kulinda amani na silka za kizanzibar. Mwenye kiti huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na Masheha wa wilaya ya Wete huko ofisi ya mkuu wa Wilaya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema katika   Ramadhani ya mwakajana waligundua jumla ya vituo 14 ambavo vilikua vinapikwa mchana wa mwezi mtukufu wa ramadhani kisiwani Pemba. ‘’Hata kama mtu si muislamu lakini hatakiwi kupika na kula mchana hadharani, hivyo niwaombe Masheha kuchukuwa hatua watu ambao wanakula kinyume na taratibu zilizowekwa na Serikali,alisema. Aidha alisema katika mji wa Wete kuna vibanda ambavyo vinatumiwa na Mama ntilie kwa ajili ya kuuzia biashara zao, lakini ikifika nyakati za usiku vibanda hivyo hutumika kama ni sehemu za starehe, hivyo aliwataka masheha kuweka ulinzi shirikishi kati

WANDISHI WA HABARI WATAKA MABADILIKO KWENYE VIFUNGU VYA SHERIA AMBAVYO VINANYIMA UHURU WA HABARI

Image
    NA FATMA HAMAD,PEMBA                                                                 Wandishi wa habari wametakiwa kutumia taluma yao kwa kuvisemea vipengele vilivyomo kwenye sheria za habari ambavyo vimekuwa vikiwandamiza wandishi pamoja na vyombo vya habari katika utekelezaji wa kazi zao ili viweze kurekebishwa. Hayo yamesemwa na Shifaa Said Hassan kutoka baraza la Habari Tanzania [MCT] wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wandishi wa habari kuhusu masuala ya habari yaliofanyika ukumbi wa TAMWA Mkanjuni Chake chake Pemba. Alisema miongoni mwa vifungu ambavyo vimekuwa ni kikwazo kwa wandishi wa habari ni kifungu cha 4, na kifungu cha 27[1] vya sheria ya Usajili wa wakala wa habari Magazeti na vitabu No 5 ya mwaka 1988 iliyo rekebishwa na sheria no. 8 ya mwaka 1997. Aidha aliendelea kufahamisha kuwa vifungu vengine ambavyo vimekua ni kikwazo kwa wandishi wa habari pamoja na vyombo vya habari ni kifungu cha 6 [1] na 7[1] vya sheria ya Tume ya Utangazaji No. 7 ya mwaka

UTELEKEZWAJI WA WANAWAKE UNAVYOCHANGIA KUONGEZEKA KWA UDHALILISHAJI

Image
      NA FATMA HAMAD,PEMBA Utelekezwaji wa Wanawake na Watoto imedaiwa ni moja ya sababu inayo changia kutokea kwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia   ikiwemo kubakwa, kulawitiwa, kwa watoto. Hayo yamesemwa na hakimu wa Mahakama maalumu ya kupambana na Udhalilishaji iliyopo Wete, Muumin Ali Juma wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano malumu wa kuwaelimisha Wananchi umuhimu wa kuripoti na kutoa ushahidi Mahakamani huko Chamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema wilaya ya Micheweni ni moja   ya wilaya inayongoza kwa utelekezaji wa wanawake, katika mkoa wa Kaskazini Pemba   jambo ambalo   linachangia   watoto kudhalilishwa. ,,Unamuacha mwanamke na watoto humpi huduma yoyote jee umetegemea nini, niwaulize wanaume wenzangu kesho mbele ya Mungu tutakwenda kujibu nini,aliuliza. Alisema   mara nyingi kesi   zinazofikishwa mahakamani   za waliofanyiwa udhalilishaji ni watoto ambao wamekosa malezi ya pamoja kati ya Baba na Mama, hivyo aliwataka wananchi ha

MIUNDO MBINU MIBOVU YA SKULI YA PUJINI KERO KWA WANAFUNZI SKULINI HAPO

Image
      NA FATMA HAMAD, PEMBA Walimu wa Skuli ya msingi Pujini wilaya ya Chake chake mkoa wa Kusini Pemba wametoa ya moyoni juu ya uwepo wa   miundombinu mibovu, pamoja na uhaba wa madarsa ya kufundishia Wanafunzi wao. Wakizungumza mbele ya viongozi wa jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chake chake wamesema baadhi ya madarsa yanavuja jambo linalopelekea kipindi cha mvua kushindwa kuendelea na vipindi kutokana na kukosa sehemu ya kufundishia. ,,Tunakilio Skuli yetu inavuja ikinyesha mvua inabidi tutafute sehemu tujifiche mpaka mvua ipite ndio tuendelee na vipindi, walieleza. Aidha walisema kuwa bado wanachangamoto ya uhaba wa vyumba vya kufundishia, hivyo wanahitaji kusaidiwa kuezekewa jingo lao ambalo tayari walishalijenga. Badhi ya wanafunzi wanaosoma Skulini hapo wamesema darasa moja lina zaidi ya wanafunzi 80,hivyo wameutaka uongozi huo kuwafanyia msaada wa kuwezekea pamoja na kuwajengea madarasa mengine jambo ambalo litaondosha usumbufu kwa wanafunzi pamoja na

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUWANZISHA MIRADI AMBAYO ITAWALETEA MAENDELEO

Image
      NASALIM HAMAD PEMBA. Kaimu mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Micheweni [Midipao] Saleh Hamad Juma amewataka wajasiriamali kuanzisha miradi kama vile utengenezaji wa Sabuni,Ukulima wa mboga ili waweze kujipatia faida itakao saidia kuendesha vikundi vyao. Ushauri huo ameutoa wakati akizungumza na wanakikundi cha kueka na kukopa cha Hatusemani kilichopo   Tumbe kaliwa wilaya ya Micheweni mkoa wa Kakazini Pemba katika kikao maalumu kilichoandaliwa na jumuiya hiyo cha kuishajiisha jamii kujiunga na vikundi vya ujasiriamali. Alisema endapo watazalisha Sabini, au kujingiza kwenye kilimo cha mboga mboga watajipatia kipato na kukuza vikundi vyao kupiga hatua kimaendeleo. ‘’Niwaombe mama zangu musishie tu kuja mukiweka pesa na kuondoka, bali anzisheni miradi ili muweze kuviendeleza vikundi vyenu pamoja na kujipatia kipato ambacho kitainua maisha yenu, alisema.   Aliendelea kusema endapo watazalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitaendana na soko la dunia wanawez

.KATIBU MKUU WA CHAMA CHA CUF AMEVITAKA VYAMA VYA SIASA KUITUNZA NA KUILINDA AMANI YA NCHI

Image
      NA FATMA HAMAD, PEMBA. Katibu Mkuu wa chama cha wananchi [CUF] Hamad Masoud Hamad amevitaka Vyama Vya Siasa kufanya siasa za kistarabu ili kuepusha maafa   yanayoweza kujitokeza katika Nchi. Katibu huyo ameyasema hayo katika hafla ya kuwaombea duwa wafuasi wa chama hicho waliofariki katika Mandamano ya mwaka 2001   pamoja na wanzilishi wa chama hicho iliyofanyika Mchanga mdogo Wete Pemba. Alisema maafa yakitokea hayachagui, hivyo ni vyema Viongozi wa vyama vya siasa kuendesha siasa zao kistarabu na kwa mujibu wa taratibu na sheria zinavyoelekeza ili kuepusha migogoro isiyoyalazima. ‘’Niwaombe viongozi wenzangu tujitahidi sana katika siasa zetu ili kilichotokea mwaka 2001 tuhakikishe hakitokei tena kwenye maisha yetu ni hatari, alisisitiza Aidha aliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka mkakati madhubuti ili kuona kila mmoja anaheshimu haki ya mwenzake, jambo ambalo litasaidia kuendelea kuwepo kwa Amani na Utulivu Nch

AFISA MDHAMINI WIZARA YA UTALII PEMBA ATOA NENO KWA WANDISHI WA HABARI

Image
                                     NA FATMA HAMAD, PEMBA Afisa mdhamini   wizara ya Utalii na mambo ya kale Pemba Zuhura Mgeni amewataka Wananchi   wa Pemba pamoja na wageni kutoka nje ya Pemba kuvitembelea vivutio vya Utalii vilivyopo kisiwani humo ili waweze kuitangaza Pemba kiutalii. Akizungumza na Wandishi wa habari kutoka Chama cha wandishi wa habari [PPC] kisiwani Pemba   mara baada ya kumaliza   ziara ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo kisiwani humo. Alisema kisiwa cha Pemba hususani mkoa wa kaskazini umejaliwa na vivutio vingi vya utalii, hivyo ni vyema wananchi pamoja na wageni kuvitembelea vivutio hivyo ili viweze kuinua Pemba katika Sekta ya Utalii. ‘’Niipongeze Jumuiya ya Wandishi wa habari Pemba kwa uwamuzi muliochukuwa wa kutembelea vivutio   mbali mbali vya   Utalii vilivyopo Pemba ili muweze kuutangaza utalii kisiwani humo,alisema. Alisema sekta ya Utalii ni moja ya sekta ambayo inaisaidia Serikali kuingiza mapato, hivyo watahakikisha wanavitunza viv